Wednesday, June 20, 2012

MSAFARA WA MUGABE WAPATA AJALI
POLICE WA ZIMBABWE WAMESEMA KWAMBA MTU MMOJA ALIFARIKI NA WENGINE 15 KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOKUMBA MSAFARI WA RAIS ROBERT MUGABE.
MOJAWAPO YA MAGARI YALIOKUWA KWENYE MSAFARA HUO WA RAIS LILIGONGA BASI LA ABIRIA KARIBU NA MJI MDOGO WA ZVIMBA.
HII NI AJALI YA PILI KUFANYIKA KATIKA MUDA WA WIKI MBILI.
MSEMAJI WA POLICE WAYNE BVUDZIJENA AMESEMA AJALI HIYO ILIYOFANYIKA SIKU YA JUMAPILI KUFUATIA HATUA YA BASI HILIO KUKAIDI AMRI YA KUPISHA MSAFARA WA RAIS MUGABE.
KWA KAWAIDA RAIS MUGABE HUSAFIRI AKIWA KWENYE MSAFARA WA MAGARI KARIBU 10.
KATIKA MSAFARA WAKE PIA HUWA KUNA MAGARI YA KIFAHARI , PIKIPIKI NA MAGARI YA KIJESHI.
INASADIKIWA KWAMBA GARI LILILOHUSIKA KATIKA AJALI HIYO LILIKUWA LIKIONGOZA MFASARA HUO KUELEKEA KATIKA KIJIJI CHA RAIS MUGABE.

No comments:

Post a Comment