Wednesday, June 20, 2012

BUNGE ATAKA NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI


MBUNGE WA JIMBO LA  MUFINDI KUSINI . MENDRAD KIGOLA KUPITIA CCM AMEITAKA SERIKALI KUWAONGEZEA POSHO WENYEVITI WA VIJIJI VYOTE HAPA NCHINI NA PIA  KUZIBANA KAMPUNI KUBWA ZA WAWEKEZAJI ILI KUONGEZA KIMA CHA CHINI YA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI WAO.
“KAMA WAWEKEZAJI NA WENYE KAMPUNI KUBWA, WATASHINDWA KULIPA MISHAHARA MIZURI KWA WAFANYAKAZI, LICHA YA KUPATA FAIDA KUBWA HAINA SABABU YA KUWAACHA WAENDELEE KUVUNA UTAJIRI WA TAIFA HILI”.
 INAPASWA KAMPUNI HIZO, ZILIPE KIMA CHA CHINI ZAIDI YA SH 170,000 AMBAZO ZINATAJWA NA SERIKALI, HASA KWA KUWA WANAPATA KIPATO KIKUBWA KATIKA BIASHARA ZAO. KUTOKANA NA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI YA KWENYE MISHAHARA YA  WAFANYAKAZI  (PAYE)

“KILA MTU HAPA, AKIENDA KIJIJI ANAHITAJI KWANZA KUKUTANA NA HAWA WENYEVITI WA VIJIJI, SASA NAO LAZIMA WAGUSWE NA NYONGEZA YA MATUMIZI YA SERIKALI,” ALISEMA KIGOLA. KUTOKANA NA KUONGEZA MATUMIZI YA KAWAIDA YA SH10.5 TRILIONI SERIKALINI YAKAWAGUSA WENYEVITI WA VIJIJI KWANI NDIO CHANZO CHA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZOTE ZA SERIKALI NA HATA WABUNGE.
AKIZUNGUMZIA ONGEZEKO LA KODI YA MAWASILIANO YA SIMU, ALISEMA ITAKUWA NA ATHARI KUBWA KWA WATUMIAJI WA KAWAIDA, AMBAO SASA WANATUMIA SIMU ZAO KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI.
“KODI HII NI YA KUWANYONGA WATUMIAJI WA SIMU KWANI,TANZANIA INAONGOZA KATI YA NCHI ZOTE ZA AFRIKA YA MASHARIKI KWA KUWA NA WATUMIAJI WENGI WA SIMU”ALISEMA KIGOLA.

No comments:

Post a Comment