Monday, June 25, 2012

MOMBASA YA SHAMBULIWA


MTU MMOJA AMEUWAWA KATIKA MLIPUKO ULIOTOKEA KATIKA BAA MOJA ILIYOKO VIUNGANI MWA MJI WA MOMBASA NCHINI KENYA.
POLISI WAMESEMA ZAIDI YA WATU WANANE WAMEJERUHIWA KUFUATIA SHAMBULIO HILO LILILOTOKEA SAA NNE, JUMAPILI USIKU.
SHAMBULIO HILO LIMEJIRI SIKU MOJA BAADA YA UBALOZI WA MAREKANI NCHINI KENYA KUONYA KUWA ''KULIKUWA NA TISHO LA KUTOKEA SHAMBULIO LA KIGAIDI'' KATIKA ENEO HILO.
MAPEMA WIKI HII, MAAFISA WA POLISI WA KENYA WALIWAKAMATA RAIA WAWILI WA IRAN WALIOTUHUMIWA KUHUSIKA NA MTANDAO WA KIGAIDI UNAOPANGA KUTEKELEZA MASHAMBULIZI MJINI MOMBASA.
SIKU YA JUMAMOSI, POLISI KATIKA MJI MKUU NAIROBI, WALISEMA KUWA WALIPATA VIFAA VINAVYO SHUKIWA KUTUMIKA KATIKA KUTENGENEZA BOMU.

No comments:

Post a Comment