Friday, June 29, 2012

MGOMO WA MADAKTARI WASHIKA KASI, MADAKTARI BINGWA NAO WAJITOSA



TUKIO LA KUTEKWA NYARA, KUPIGWA NA KUJERUHIWA VIBAYA, KISHA KUTUPWA KATIKA MSITU WA PANDE ULIOPO NJE KIDOGO YA JIJI LA DAR ES SALAAM, KIONGOZI WA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA, DK STEVEN ULIMBOKA, LIMECHOCHEA KASI YA MGOMO BAADA YA MADAKTARI BINGWA KUTANGAZA KUJITOSA RASMI KWENYE MGOGORO HUO.AWALI MADAKTARI HAO HAWAKUSHIRIKI MGOMO HUO, LAKINI JANA WALIELEZA KWA NYAKATI TOFAUTI KUWA, WAMEAMUA KUUNGANA NA WENZAO KUTOKANA NA UNYAMA ALIOFANYIWA KIONGOZI WAO AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUTETEA NA KUPIGANIA HAKI ZAO.

MADAKTARI HAO WA HOSPITALI ZA MUHIMBILI, MOI, KCMC, MBEYA, BUGANDO NA OCEAN ROAD YA JIJINI DAR ES SALAAM, JANA WALITANGAZA RASMI KUWA WAMEINGIA KWENYE MGOMO HUO KUSHINIKIZA PAMOJA NA MAMBO MENGINE, SERIKALI KUTOA TAMKO KUHUSU UTATA WA TUKIO HILO.
TUKIO HILO LA AINA YAKE KUTOKEA NCHINI, LIMEATHIRI UPATIKANAJI WA HUDUMA ZOTE ZA MATIBABU KATIKA HOSPITALI HIZO, HUKU MADAKTARI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI NA MOI, WAKIELEKEZA NGUVU ZAO KUNUSURU MAISHA YA MWENZAO ALIYEUMIZWA.
KATIBU WA JUMUIYA YA MADAKTARI, DK EDWIN CHITAGE, ALIWAAMBIA WAANDISHI WA HABARI KUWA MGOMO HUO UTAENDELEA HADI HAPO SERIKALI ITAKAPOTEKELEZA MADAI YAO.

No comments:

Post a Comment