Sunday, June 10, 2012

MGOMO WA MADAKTARI WANUKIA TENA


CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA (MAT) KIMETANGAZA MGOGORO NA SERIKALI NA KUIPA WIKI MBILI KUYAPATIA UFUMBUZI MATATIZO YAO LA SIVYO WATAFANYA MGOMO WA NCHI NZIMA.  WAMETOA MSIMAMO HUO WALIPOKUTANA JANA JIJINI DAR ES SALAAM IKIWA NI SIKU CHACHE BAADA YA UJUMBE WAO ULIOKUWA KWENYE MAZUNGUMZO NA SERIKALI KUGOMA KUSAINI MAKUBALIANO KWA KILE WALICHOELEZA MPAKA WAPATE RUKSA YA WANACHAMA.  JANA ILIKUWA NI SIKU YA UJUMBE HUO KUWASILISHA TAARIFA YA MAKUBALIANO AMBAYO SERIKALI ILITAKA WAISAINI NA HIVYO WANACHAMA HAO HAWAKUYARIDHIA HIVYO KUAMUA KUTANGAZA MGOGORO.
 HABARI ZILIZOIFIKIA MWANANCHI JUMAPILI KUTOKA NDANI YA KIKAO HICHO CHA NDANI ZILIELEZA KUWA MADAI AMBAYO SERIKALI IMESHINDWA KUYATEKELEZA NI NYONGEZA YA MISHAHARA, MAZINGIRA MAZURI YA KAZI, MARUPURUPU, NYONGEZA YA POSHO YA WITO WA DHARURA, POSHO ZA NYUMBA NA CHANJO.
 MKUTANO HUO AMBAO ULIWASHIRIKISHA MADAKTARI PAMOJA NA VIONGOZI WA CHAMA HICHO WALIKUBALIANA KUTANGAZA MGOGORO WA WIKI MBILI NA BAADA YA HAPO WATAINGIA KATIKA MGOMO ILI KUISHINIKIZA SERIKALI KUYAPATIA UFUMBUZI MADAI YAO.


1 comment: