Friday, June 22, 2012

MAREKANI IINAUZUIA KUTOLEWA KWA RIPOTI


MAREKANI IINAUZUIA KUTOLEWA KWA RIPOTI MUHIMU KUHUSINA NA WAASI WANAOONGOZWA NA JENERALI WA JESHI ANAYESAKWA NA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA JINAI ICC. HII NI KWA MUJIBU WA SHIRIKA LA KUTETETEA HAKI ZA BINADAMU HUMAN RIGHTS WATCH.
SHIRIKA HILO LIMESEMA MAREKANI IMEKUWA IKIPINGA KUTOLEWA KWA RIPOTI YA HARAKATI ZA WAASI WANAOONGOZWA NA BOSCO NTAGANDA MASHARIKI MWA JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.
TAYARI UMOJA WA MATAIFA UMETOA TAARIFA INAYOANGAZIA JINSI RWANDA AMBAYO NI MSHIRIKA WA KARIBU WA MAREKANI IMEKUWA IKIFADHILI WAASI MASHARIKI MWA CONGO.
HATA HIVYO MAREKANI IMEKANUSHA KUZUIA KUTOLEWA KWA RIPOTI HIYO.RIPOTI HIYO ILITARAJIWA KUTOLEWA SIKU KADHAA ZILIZOPITA NA JOPO MAALUM{GROUP OF EXPERTS}.
VUGUVUGU LA SASA LINAONGOZWA NA JENERALI BOSCO NTAGANDA ALIYEASI JESHI LA CONGO PAMOJA NA BAADHI YA MAAFISA WENGINE WA JESHI.
NTAGANDA AMERIPOTIWA KUDHIBITI ENEO KARIBU NA MPAKA NA RWANDA. MAKUNDI MENGI YA WAASI WA CONGO YAMEKUWA YAKIFADHILI HARAKATI ZAO KUTOKANA NJIA ZA MAGENDO HUSUSAN MAUZO YA MADINI.
MAELFU YA RAIA MASHARIKI MWA CONGO WAMEKIMBIA MAKAAZI YAO KUTOKANA NA HARAKATI ZA JESHI LA SERIKALI NA MAKUNDI YA WAASI.

No comments:

Post a Comment