Friday, June 8, 2012

MAANDAMANO YA SHURA YA MAIMAMU YAZUILIWA


JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEZUIA MAANDAMANO YA SHURA YA MAIMAMU TANZANIA YALIYOPANGWA JIJINI LA DAR ES SALAAM KUPINGA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA (NECTA) KUTOKANA NA KASORO ILIYOJITOKEZA KATIKA MTIHANI WA DINI HIYO WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2012.
MAANDAMANO HAYO YALIPANGWA KUANZIA SEHEMU MBALIMBALI ZA JIJI HILO NA KUISHIA VIWANJA VYA KIDONGO CHEKUNDU.
KAIMU KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM, AHMED MSANGI ALISEMA JESHI HILO HALIONI SABABU YA KUFANYIKA KWA MAANDAMANO HAYO BADALA YAKE AMEWATAKA WAHUSIKA KUFANYA  MKUTANO PEKE YAKE KATIKA VIWANJA HIVYO.
ALISEMA SABABU ZA KUSITISHA MAANDAMANO HAYO NI UGUMU KWA JESHI LA POLISI KUTOA ULINZI KWA SABABU WAUMINI WANATOKEA KATIKA MISIKITI MBALIMBALI, HIVYO WANGESHINDWA KUYADHIBITI, ENDAPO PANGETOKEA VURUGU.
MAPEMA, WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI, DK SHUKURU KAWAMBWA ALIWATAKA WANANCHI KUTOSHIRIKI MAANDAMANO HAYO KWA SABABU SUALA WALILOKUWA WAKILALAMIKIA LIMESHAFANYIWA KAZI NA WIZARA PAMOJA NA NECTA.

No comments:

Post a Comment