Friday, June 8, 2012

FAIDA ZA MATUNDA MBALIMBALI



 zabibu
UTAFITI MPYA ULIOFANYIKA NCHINI MAREKANI UMESEMA YA KWAMBA KULA MACHUNGWA NA ZABIBU KUNAWEZA KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KIHARUSI (STROKE).
UTAFITI HUO ULIANGALIA FAIDA ZA MATUNDA CHACHU (CITRUS FRUIT) PEKEE KWA MARA YA KWANZA TOFAUTI NA TAFITI NYINGI AMBAZO TUMEZIZOEA ZINAZOANGALIA UMUHIMU WA MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI KWA AFYA KIUJUMLA.
machungwa

UTAFITI HUU UMEHUSISHA MAELFU YA WANAWAKE WANAOSHIRIKI KATIKA TAFITI YA MANESI NURSE’S HEALTH STUDY LAKINI WATAALAMU WANAAMINI FAIDA HIZO ZA MACHUNGWA NA ZABIBU PIA ZINAPATIKANA KWA WANAUME.
TIMU YA WATAFITI KATIKA CHUO CHA NORWICH MEDICAL SCHOOL KATIKA CHUO KIKUU CHA EAST ANGLIA WAMECHUNGUZA UMUHIMU WA KEMIKALI AINA YA FLAVONOIDS AMBAYO NI JAMII YA ANTIOXIDANT (KEMIKALI ZINAUWA KEMIKALI HATARI ZA KWENYE MWILI) INAYOPATIKANA KATIKA MATUNDA, MBOGA ZA MAJANI, CHOCOLATE NYEUSI NA WINE NYEKUNDU.
UTAFITI HUU ULIFUATILIA TAKWIMU ZA MIAKA 14 ZA WANAWAKE 69,222 AMBAO WALIKUWA WAKISHIRKI KATIKA TAFITI KWA KUANDIKA KIWANGO CHAO CHA KULA MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI KWA KILA KIPINDI CHA MIAKA 4. TIMU HIYO YA UTAFITI ILIANGALIA UHUSIANO WA AINA SITA YA FLAVONOIDS - FLAVANONES, ANTHOCYANINS, FLAVAN-3-OLS, FLAVONOID POLYMERS, FLAVONOLS NA FLAVONES NA HATARI YA AINA MBALIMBALI ZA KIHARUSI KAMA ISCHAEMIC, HEMORRHAGIC NA TOTAL STROKE. ILIONEKNA WANAWAKE WALIOKULA KIWANGO KIKUBWA CHA FLAVANONES KWENYE MATUNDA CHACHU WALIKUWA NA ASILIMIA 19 YA UWEZEKANO WA KUPUNGUZA KIHARUSI KULINGANISHA NA WANAWAKE AMBAO WALIKULA KIWANGO KIDOGO CHA MATUNDA HAYO.

No comments:

Post a Comment