Saturday, June 9, 2012

HATUTA WAJIBU CHADEMA LEO - NAPE


KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), NAPE NNAUYE AMESEMA CHAMA CHAKE HAKINA MPANGO WA KUUTUMIA MKUTANO WAKE WA LEO KWENYE VIWANJA VYA JANGWANI KUJIBIZANA NA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA BADALA YAKE, KITAJIKITA ZAIDI KATIKA KUTOA SOMO KWA WAJUMBE WAPYA WA MASHINA NA VIONGOZI WA MATAWI MKOA WA DAR ES SALAAM.


KAULI HIYO YA NAPE INATOA MTAZAMO TOFAUTI NA TETESI KWAMBA  CCM KITATUMIA MKUTANO HUO KUKIJIBU CHAMA HICHO KIKUU CHA UPINZANI AMBACHO NACHO KILIFANYA MKUTANO KWENYE VIWANJA HIVYO HIVI KARIBUNI.
KATIKA MKUTANO HUO AMBAO CHADEMA KILIZINDUA MPANGO WAKE WA VUGUVUGU LA MABADILIKO (M4C) MWISHONI MWA MWEZI ULIOPITA, KILIORODHESHA SHUTUMA NYINGI DHIDI YA SERIKALI YA CCM ZIKIWEMO ZA KUSABABISHA MAISHA MAGUMU KWA WATANZANIA.

No comments:

Post a Comment