Saturday, June 9, 2012

CHADEMA MKOANI PWANI


.
BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/12/06/09/10:33:28

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO MKOA WA PWANI, KINAFANYA MKUTANO WA HADHAR WILAYANI MAFIA KATIKA VIWANJA VYA KILINDONI IKIWA NI SEHEMU YA KUJIIMARISHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015.

KWA MUJIBU WA CHADEMA MKOA WA PWANI, BW. SAID UKWEZI AMESEMA KATIKA KUHAKIKISHA SERA ZA CHAMA CHAKE ZINAFIKA KATIKA KILA KONA YA MKOA WA PWANI, WAMEELEKEZA NGUVU ZAO KATIKA WILAYA AMBAYO NI NGOME YA CHAMA CHA CUF, ILI KUWAPATIA UKOMBOZI KUPITIA MSEMO WAO WA "VUA GAMBA VAA GWANDA".

BW. UKWEZI AMEFURAHISHWA NA MAPOKEZI MAKUBWA AMBAYO WAMEYAPATA KISIWANI HAPO YAKIONGOZWA NA MWENYEKITI WA WILAYA WA CHAMA HICHO BW. ALLY MOHAMED KIGOMBA.

WAKATI MKUTANO WA HADHARA WA CHADEMA UNAFANYIKA WILAYANI MAFIA LEO, MJINI KIBAHA KESHO MHESHIMIWA TINDU LISSU ANATARAJIWA KUWAHUTUBIA WANANCHI WA WILAYA YA KIBAHA VIJIJINI HAPO KESHO KWENYE VIWANJA VYA STENDI YA MZENGA KATIKA UTEKELEZAJI WA KAMPENI YAO YA MOVEMENT FOR CHANGE.

MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA PWANI BW. ELLISON KINYAHA AMESEMA LENGO LA MKUTRANO HUO NI KUWAPA FURSA WANANCHI KUJUA NA KUZIELEWA SERA ZA CHADEMA NA MIKAKATI YAKE ILIYONAYO KATIKA KUKIJENGA NA KUKIIMARISHA CHAMA HICHO KIKIJIANDAA KUCHUKUA DOLA MWAKA 2015 HASA KWA KUZINGATIA FURSA KADHAA AMBAZO ZIPO BAYANA IKIWA PAMOJA NA CHAMA TAWALA KUSHINDWA KUTIMIZA MATAKWA YA WANANCHI AMBAO NDIO WAPIGA KURA.

AIDHA BW. KINYAHA AMEKANUSHA KUWA KAMPENI YA MOVEMENT FOR CHANGE KUWA INAAMBATANA NA VITENDO VYA VURUGU, AMBAPO SIKU ZOTE CHAMA CHAO KIMEKUWA KIKIFANYA MAMBO YAKE BILA KUWEPO KWA UVINJIFU WA AMANI, AMESEMA SHUTUMA HIZO NI MBINU YA BAADHI YA WASIOITAKIA MEMA CHADEMA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KISIASA.


No comments:

Post a Comment