Monday, June 11, 2012

HAMILTON AFANYA MAMBO


LEWIS HAMILTON ALIFANIKIWA KUWA MSHINDI KATIKA MASHINDANO YA JUMAPILI YA GRAND PRIX, AKIANDIKISHA REKODI YA MASHINDANO MSIMU HUU KUSHUHUDIA WASHINDI MBALIMBALI WA MSIMU HUU, AKIWA NI MSHINDI WA SABA, KWA USHINDI HUO WA CANADA.
Lewis Hamilton

MUINGEREZA HAMILTON, AMBAYE NI DEREVA WA TIMU YA MCLAREN, ALIMTANGULIA ROMAIN GROSJEAN, DEREVA WA RENAULT, NA SERGIO PEREZ, DEREVA WA SAUBER, NA ALIYEMALIZA KATIKA NAFASI YA TATU.
HUKU IKISALIA MIZUNGUKO KUMI KABLA YA MASHINDANO KUMALIZIKA, HAMILTON ALIPAMBANA KUTOKA NAFASI YA TATU HADI YA KWANZA, NA AKIFANIKIWA KUMPITA DEREVA WA FERRARI, FERNANDO ALONSO, NA PIA WA RED BULL, SEBASTIAN VETTEL.
MADEREVA HAO WAWILI WALIAMUA KUSIMAMA MARA MOJA KWA MAGARI YAO KUKAGULIWA, WAKIDHANI MBINU HIYO ITAWASAIDIA, HUKU HAMILTON AKISIMAMA MARA MBILI.
HUU NI USHINDI WA TATU WA HAMILTON KATIKA BARABARA ZA GILLES VILLENEUVE, NA USHINDI HUO UNAMWEZESHA KUONGOZA KWA POINTI KATIKA KUWANIA UBINGWA WA MSIMU HUU WA MWAKA 2012, AKIMSHINDA ALONSO KWA POINTI MBILI, NA VETTEL, KATIKA NAFASI YA TATU, 

No comments:

Post a Comment