Sunday, June 10, 2012

BOB MAKANI MWASISI WA CHADEMA AFARIKI DUNIAMWASISI wa Chadema na Mwanasheria mkongwe nchini Bob Makani, amefariki dunia usiku katika hospitali ya Aga khan, jijini Dar es Salaam.


Januari 17 mwaka huu katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema Regia Mtema, Makani alianguka muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa marehemu.

 Baada ya tukio hilo, alibebwa na kupelekwa pembeni ambako alipepewa kwa takriban dakika tano kisha kurejea katika hali yake ya kawaida na kurudi kwenye kiti chake

Alikuwa Katibu Makuu wa kwanza wa Chadema kati ya mwaka 1993 hadi 1998, alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho kuanzia mwaka 1998 hadi 2004 na amegombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa mara tatu kati ya mwaka 1995 na 2000 na mwaka 2005.

Kazi ambazo amewahi kuzifanya serikalini; alikuwa naibu mwanasheria mkuu wa serikali, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mwaka 1966 na elimu yake ana shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu Cha Makarere nchini Uganda.

Ni mzaliwa wa Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga akitokea kwenye ukoo wa kichifu wa Makani. <

No comments:

Post a Comment