Tuesday, June 19, 2012

HAMAD RASHID AFUNGUKA BUNGENI KUHUSU MWEKEZAJI


MBUNGE WA WAWI (CUF), HAMAD RASHID MOHAMED JANA ALIILIPUA KAMPUNI YA MADINI YA MINERALS EXTRACTIONS TECHNOLOGIES LTD KUTOKANA NA MMILIKI WAKE KUFANYA BIASHARA ZA MADINI KWA NJIA ZA UTAPELI NA UJASUSI.
MINERALS EXTRACTIONS TECHNOLOGIES LTD NI KAMPUNI AMBAYO INAFANYA KAZI YA KUSAFISHA MCHANGA WA DHAHABU KATIKA BAADHI YA MIGODI ILIYOPO KANDA YA ZIWA NA ILIWAHI KULALAMIKIWA KWA KUKATAA KUSHIRIKIANA NA MPANGO WA KUFUATILIA MAPATO YANAYOLIPWA KWA SERIKALI NA KAMPUNI ZA MADINI, GESI NA MAFUTA (TEIT) UNAOONGOZWA NA JAJI MSITAAFU, MARK BOMANI.
KUTOKANA NA HALI HIYO, MOHAMED ALITOA MAPENDEKEZO YA KUUNDWA KWA KAMATI YA WABUNGE SITA KUTOKA KAMATI TATU ZA BUNGE ILI KUCHUNGUZA KAMPUNI HIYO NA MMILIKI WAKE AMBAYE (JINA TUNALIHIFADHI KWA SASA) AMBAYE ALISEMA KUWA ANATAMBA KWAMBA TANZANIA HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUMGUSA.
AKICHANGIA HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI YA 2012/2013, MOHAMED ALISEMA MWEKEZAJI HUYO ANAMILIKI HATI TANO ZA KUSAFIRIA, TATU KUTOKA NCHINI KWAKE BELGIUM NA MBILI ZA BURUNDI NA KWAMBA BADO ANAISHI NCHINI LICHA YA KUFUKUZWA NCHINI NA SERIKALI.

No comments:

Post a Comment