Thursday, June 28, 2012

CHAMA CHA WASIOONA WILAYA YA KIBAHA NA MAOMBI YAO SERIKALINI


Ben Komba/Pwani-Tanzania/06/28/2012/8:56:13

CHAMA CHA WASIOONA WILAYA YA KIBAHA KIMEIOMBA SERIKALI KUTOA MACHAPISHO KUHUSIANA NA ELIMU YA SHERIA YA KUZUIA NA KUDHIBITI UKIMWI KWA KUTUMIA MNAANDISHI YA NUKTA NUNDU ILI KUWAWEZESHA KUIFAHAMU NA KUIELEWA IPASAVYO SHERIA HIYO KWA FAIDA YAO.

MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA WASIOONA TANZANIA, ROBERT BUNDALA AMESEMA KWA MUDA MREFU WAMEKUWA WAKITAFUTA MBINU YA KUHAKIKISHA MACHAPISHO YOTE NA MAJARIDA YANALENGA KUIPATIA JAMII UJUMBE WA AINA YOYOTE, WAMETAKA SERIKALI NAYO ISIWASAHAU KWA KUTOA MACHAPISHO KWA KUTUMIA HATI YA NUKTA NUNDU ILI KULIWEZESHA KUNDI HILO KWENDA SAWA NA MAKUNDI MENGINE KATIKA KUPATA TAARIFA MUHIMU.

BW. BUNDALA AMEIFAHAMISHA SERIKALI NA JAMII KUWA WAO KAMA WALEMAVU WA MACHO, LAKINI SEHEMU NYINGINE ZA MIILI YAO IPO KAMILI KAMA BIMNADAMU MWINGINE YOYOTE, HIVYO KUWAFANYA NA WAO KUWA KATIKA MOJA YA MAKUNDI AMBAYO YAPO KATIKA HATARI YA KUPATA MAAMBUKIZI, NA HASA KUTOKANA NA KUKOSA TAARIFA MUHIMU KUNAKOSABABISHWA NA ULEMAVU WALIONAO, NA NJIA PEKEE YA KUWAOKOA NI KWA SERIKALI KUTUMIA NUKTA NUNDU KUFIKISHA ELIMU HII KWAO.

AMESEMA CHAMA CHA WASIOONA TANZANIA KIMEKUWA KIKISHIRIKIANA NA ASASI NYINGINE KADHAA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA HATARI WA UKIMWI, NA AMECHUKUA NAFASI HIYO KUMSHUKURU, MWAKILISHI WA TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA, TACAIDS MKOA WA PWANI, BW. HAFIDH AMIR KWA KUWA KARIBU SANA NA CHAMA CHAO.

AKIONGEA KATIKA MDAHALO HUO, MWAKILISHI WA MKUU WA MKOA, MKUU WA WILAYA YA KIBAHA, HAJAT HALIMA KIHEMBA AMEWATAKA WATU WASIOONA KUJIEPUSHA NA MAJANGA YASIYO NA LAZIMA HASA KUTOKANA NA BAADHI YAO KUENDEKEZA STAREHE PAMOJA NA HALI YAO KUWA HIVYO, AMBAPO BAADHI YAO WANADIRIKI KWENDA MAENEO YA STAREHE MPAKA MUDA WA USIKU KWANI MAENEO HAYO MARA NYINGI UWA NA MAMBO YA KISHETANI YANAYOWEZA KUHATARISHA MAISHA YAO.

AIDHA AMEWATAKA WATU WASIOONA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA ZOEZI LA SENSA YA MAKAZI, NA KUPUUZA JARIBIO LOLOTE LA KUSUSIA ZOEZI HILO KWA KISINGIZIO CHA DINI, KWANI KUENDEKEZA MAMBO KAMA HAYO YA UDINI NDIO CHANZO CHA MIGOGORO MBALIMBALI ULIMWENGUNI AKATOLEA MFANO NCHI YA NIGERIA NA SUDAN.

No comments:

Post a Comment