Sunday, June 17, 2012

CHADEMA , CCM TOFAUTI KANDO MASLAHI YA TAIFA KWANZA


WANACHAMA WA CCM NA CHADEMA WILAYANI NZEGA MKOANI TABORA JANA WALIWEKA PEMBENI TOFAUTI ZAO ZA KISIASA NA KUANDAMANA KWA PAMOJA KUUSHINIKIZA UONGOZI WA MGODI WA RESOLUTE KUTEKELEZA AHADI WALIZOAHIDI WAKATI WAKIKABIDHIWA MGODI HUO  MIAKA MITATU ILIYOPITA.

MAANDAMANO HAYO YALIYOANZIA NZEGA MJINI HADI KIJIJI CHA NATA KILICHOPO NJE KIDOGO YA MJI HUO YALIANDALIWA NA MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA, DK HAMIS KIGWANGALLAH.
 

YALIFANYIKA BAADA YA WAMILIKI WA MIGODI HIYO KUSHINDWA KUTEKELEZA AHADI ZA UJENZI WA SHULE, ZAHANATI PAMOJA NA KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA ENEO HILO.

WANACHAMA WA CHADEMA WALIONEKANA WAKIWA NA BENDERA ZA CHAMA HICHO HUKU WAKIONYESHA ISHARA YA VIDOLE VIWILI AMBAYO HUTUMIWA NA CHAMA HICHO KIKUU CHA UPINZANI NCHINI.

PAMOJA NA POLISI KUTANDA KILA KONA WAANDAMANAJI HAO WALIOKUWA NA BENDERA HUKU WAMKITEMBEA KWA MIGUU NA BAADHI WAKIWA KATIKA MAGARI, WALIINGIA KATIKATI YA KUNDI LA WANACHAMA WA CCM NA KUANZA KUTEMBEA KUELEKEA KATIKA KATIKA KIJIJI CHA MWABANGU AMBAPO ULIFANYIKA MKUTANO HUO.

No comments:

Post a Comment