Sunday, June 17, 2012

BAJETI YAPINGWA NA MCHUMI PROF LIPUMBA


MWENYEKITI WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF), PROFESA IBRAHIM LIPUMBA AMEUNGANA NA WENYEVITI WA VYAMA VINGINE VYA SIASA VYA UPINZANI KUPINGA BAJETI YA SERIKALI YA 2012/2013, AKISISITIZA KUWA KAMWE CHAMA CHAKE NA WABUNGE WAKE, HAWATAIUNGA MKONO.

KWA KAULI HIYO, LIPUMBA AMEUNGANA NA WENYEVITI WENZAKE WA VYAMA VYA UPINZANI, FREEMAN MBOWE WA CHADEMA NA JAMES MBATIA WA NCCR-MAGEUZI AMBAO PIA WALIIPONDA BAJETI HIYO WAKISEMA HAINA JIPYA.
KWA UPANDE MWINGINE, WABUNGE WA CCM JUZI WALIKUTANA KWA ZAIDI YA SAA TANO KATIKA KIKAO AMBACHO WALIIBUA HOJA YA KUTAKA KUCHUNGUZWA KWA MFUKO MKUU WA SERIKALI KWA MAELEZO KWAMBA KUNA DALILI ZA KUWAPO UFISADI.

HABARI KUTOKA NDANI YA KIKAO HICHO  KILICHOONGOZWA NA WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA ZINASEMA MSINGI WA HOJA HIYO ILIYOTOLEWA NA MBUNGE WA SIMANJIRO, CHRISTOPHER OLE SENDEKA NA KUUNGWA MKONO NA WABUNGE WENGINE, NI KUTOKUWAPO KWA UWIANO KATI YA FEDHA ZILIZOKUSANYWA NA MAMLAKA YA MAPATO (TRA) PIA KUTOKA KWA WAHISANI NA ZILE ZILIZOPELEKWA KATIKA WIZARA NA IDARA ZA SERIKALI.

No comments:

Post a Comment