Friday, May 18, 2012

WIGAN YATOA REHUSA MAJOGOO WA JIJI WAZUNGUMZE NA MARTINEZ

Wigan imeiruhusu klabu ya Liverpool kushauriana na meneja Roberto Martinez, ikiwa atakubali kuiongoza klabu hiyo ya uwanja wa Anfield.
Roberto Martinez
Liverpool kujaribu kumvuta aingie Anfield
Tajiri wa Wigan, Dave Whelan amethibitisha habari hizo.
Kenny Dalglish, aliyekuwa meneja, alifutwa kazi siku ya Jumatano, na klabu ya Liverpool inamtafuta kocha wa nne katika kipindi cha miaka miwili.
"Nilitoa idhini kwa Liverpool kuzungumza na Roberto na watazungumza naye hivi punde", Whelan aliwaelezea waandishi wa habari wa michezo wa Sky.
Uongozi wa Liverpool umo katika kuwatafuta watu ambao huenda wakafaa kuchukua kazi hiyo, ikiwa ni pamoja na meneja wa Swansea, Brendan Rodgers.
Martinez alikuwa meneja wa Swansea mwezi Februari, mwaka 2007, na kuiwezesha timu kufika hadi daraja ya kwanza.
Whelan amesema anatumaini Martinez ataamua kusalia katika uwanja wa DW, lakini anafahamu umaarufu wa meneja huyo Mhispania.
"Sijui Roberto ana hisia zipi kuihusu klabu ya Liverpool.
Nadhani atakuwa akielekea huko akiwa tayari kwa lolote.
Lakini ningelipenda Roberto kubaki".

No comments:

Post a Comment