Mchezaji mashuhuri wa timu ya
Italia na klabu ya Juventus, Alessandro Del Piero anatazamiwa kucheza
mechi yake ya mwisho jumapili hii dhidi ya Napoli katika fainali
ijulikanayo kama Coppa Italia mbele ya umati wa watu kwenye uwanja wa
Stadio Olimpico mjini Rome.
Del Piero mwenye umri wa miaka 37 akiwa ni
nahodha wa klabu ya Juventus ni shujaa wa mjini Turin, na katika kipindi
chake amefunga mabao 290 katika mechi 704 aliyoshiriki, ingawa bodi ya
klabu yake haijamuongezea mkataba na huenda akaelekea Marekani msimu
ujao.Katika kipindi cha miaka 19 ya uchezaji wake, Del Piero ameshinda Ligi ya Serie A mara sita, kombe led Coppa Italia mara moja, Ligi ya mabingwa na kombe la Kimataifa la kombe la Ligi za mabingwa duniani pamoja na Kombe la Dunia la mwaka 2006.
Wiki iliyopita, aliaga mashabiki wake na Ligi ya Serie A ambapo aliweza kufunga katika mechi ya Juventus dhidi ya Atalanta 3-1 na klabu yakew kujitokeza kua ya tatu kumaliza msimu wa Ligi bila kupoteza.
Del Piero aliondolewa katika kipindi cha pili, akiitikia mwaliko wa kusimama mbele ya uwanja wa Juventus, eneo maarufu la Curva Sud akiwapungia mkono mashabiki waliojaa machozi, kabla ya kuelekea upande wa pili wa uwanja kupokea shangwe za mashabiki.
No comments:
Post a Comment