Thursday, May 31, 2012

ubaguzi wa rangi michezoni

Mario Balotelli

Mario Balotelli nyota wa soka nchini Italia ambaye pia ni mchezaji mweusi wa Klabu ya Manchester City ya Uingereza amesema ataondoka uwanjani endapo atakejeliwa kutokana na rangi yake wakati wa mchuano wa kombe la Mataifa Ulaya katika nchi za Poland na Ukraine mwezi Juni.

Matamshi yake yanatokea kufuatia makala ya BBC ambayo yaliangazia ghasia katika viwanja vya soka kutokana na ubaguzi wa rangi katika nchi hizo mbili.

Makala hayo yalionyesha mashabiki wakizungu wakiwakejeli wachezaji weusi na kuwashambulia mashabiki wenye asilia tofauti na kizungu.

Wanasiasa na maafisa wa soka kutoka nchi hizo wamesema tatizo hilo limetiwa chumvi.

Kukejeliwa kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya Balotelli nchini Italia mwaka 2009 kulifanya shirika la soka Ulaya UEFA kuweka sheria ya kuwalazimisha marefa kusimamisha mechi ikiwa kejeli za ubaguzi wa rangi zitaendelea.

No comments:

Post a Comment