Thursday, May 31, 2012

majeshi ya kenya


Ramani ya Kenya na Somalia ikionyesha mji wa Afmadow
Wanajeshi wa Kenya wakisaidiana na majeshi ya serikali ya Somalia wameuteka mji muhimu wa Afmadow uliodhibitiwa na kundi la kiisilamu la Al Shabaab.
Wanajeshi hao waliingia eneo hilo bila upinzani wowote.Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali ameambia BBC kutekwa kwa mji wa Afmadow kunatoa nafasi kubwa kwa wanajeshi katika harakati za kulitwaa eneo la bandari la Kismayo ambalo ni ngome kuu ya Al Shabaab.
Bandari ya Kismayo inatumika na Al Shabaab kuvukisha silaha na ushuru unaotozwa wawekezaji wanaotumia bandari hiyo kuleta bidhaa nje na kutuma nje ya Somalia.

No comments:

Post a Comment