Wednesday, May 16, 2012

SALUM HAMIS aka UKAGIRI au MAPOZI ameuwawa

Ben Komba/Pwani- Tanzania/Thursday, May 03, 2012/12:23:48

Jambazi aliyejulikana kwa jina la SALUM HAMIS aka UKAGIRI au MAPOZI ameuwawa kwa kupigwa risasi kufuatia tukio la kurushiana risasi na Polisi baada ya kubainika kufanya kitendo cha uhalifu katika kijiji cha Vikuge wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa kuvamia duka la Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi wilayani Kibaha mkoa wa Pwani, BW. UWESU ABDALLAH.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Afisa habari Mkoa wa Pwani, Inspekta ATHUMAN MTASHA zimebainisha kuwa majira ya saa saba usiku (01:00hrs) huko Kijiji cha Vikuge Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani. Majambazi yanayokadiriwa kuwa kumi walivamia nyumbani kwa UWESU ABDALLAH, mwenye umri wa miaka 75 na kuvunja kwenye duka lake na kuiba.

Wakati wanatenda kosa hili walimchoma visu mwenye nyumba sehemu za tumboni na kichwani na kusababisha kifo chake. Vile vile walimjeruhi mke wa marehemu aitwaye ZUWENA KONDO, mwenye umri wa miaka 50 sehemu za sehemu za mkono wa kulia na kichwani . Majambazi hao walifanikiwa kupora vifaa mbalimbali vya dukani na kutoweka.


Polisi waliokuwa doria eneo la Vikuge walisikia mlio wa bunduki na ndipo walipoelekea eneo la tukio hili. Wakati wanakaribia kwa mbali waliwaona majambazi hao wakitokea eneo la tukiowakiwa na tochi nyingi na ndipo walipowashambulia kwa risasi. Polisi walifamikiwa kuua jambazi mmoja ajulikanaye kwa jina la SALUMU HAMIS @ UKAGIRI au MAPOZI, mwenye umri wa miaka 30 na mkazi wa Kijiji cha SOGA.

Jambazi hili lilikuwa linatafutwa na Polisi kwa kuhusika na tukio la Unyang’anyi wa kutumia silaha uliotokea tarehe 27/03/2012 nyumbani kwa HERI MATHIAS NGOTA wa Kijiji cha Vikuge. Jambazi hilin lilikutwa na kiroba kilichokuwa na vifaa mbalimbali vilivyoibiwa kwenye duka la marehemu UWESU ABDALLAH.

Juhudi za kuwasaka Majambazi wengine waliokimbia baada ya kukurupushwa na Polisi zinaendelea.

Marehemu UWESU ABDALLAH kabla hajajiunga na chama chama cha CUF aliwahi kuwa Diwani wa CCM, na ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe waliokuwa wanazifahamu barabara duru za kisiasa nchini, tunamuomba mwenyezi Mungu mwanga wa milele amuangazie na astarehe kwa amani.

No comments:

Post a Comment