Wednesday, May 16, 2012

MAENDELEO KIBAHA

Ben Komba/ Pwani- Tanzania/05/14/12/18:43:40

Katika hatua ya kuhakikisha vijana mkoani Pwani wanapata stadi za maisha, shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE linatoa mafunzo kwa wanawake vijana ambayo yamelenga kuwainua kaitka masuala ya stadi za biashara na uchumi ili waweze kupunguza utegemezi.


Mratibu wa mafunzo hayo ya siku saba, BI.GROLIA MABELE amesema mafunzo hayo y
anawahusisha vijana 20 kutoka Kibaha mjini na Kibaha vijijini na yanajulikana kama WANAWAKE VIJANA UHURU NA MABADILIKO (WAVUMA), ambapo wanawake hao vijana wataenda kuwa wawezeshaji kwa wenzao ambao wapo katika kata zao.

BI.MABELE ameongeza matarajio yake baada ya mafunzo hayo ya ujasiriamali watakayopatiwa wanawake hao vijana yatawasaidia kwa njia moja au nyingine kwa kuanzisha miradi ambayo itawasaidia kiuchumi na kuwawezesha kuto mchango katika familia zao pale itakapohitajika,

Aidha amewashauri wafadhili ambao wanawezesha kuwepo mafunzo hayo kujenga mahusiano na taasisi nyingine ili ziweze kusaidia, kutafuta namna ambayo itawezesha vijana hao kupata japo mitaji mara wanapomaliza mafunzo, katika kuwezesha mafunzo hayo kutumika kwa faida badala ya washiriki kutoenda kutum,ia ipasavyo mafunzo hayo kwa faida ya jamii.

Naye mwezeshaji kutoka mradi wa vijana wa Kazi nje nje unaofadhiliwa na shirika la kazi Duniani-ILO-, BW. EDWIN MENGISTU amewaambia washiriki kuwa sifa ya majasiriamali ni kuwa mbunifu wa kuanza na kuendeleza biashara kwa lengo la kujipatia kipato na kufanikiwa.

BW. MENGISTU amefafanua mjasiriamali yoyote anatakiwa kutambua na kutumia fursa au kero na kuzitumia ipasavyo katika kuhakikisha wanajiletea maendeleo endelevu kwa kupitia shughuli anayofanya, na uaminifu ukiwa ndio dira kuu kutokana na shughuli za kijasiriamali m,ara nyingi kuhusisha mitandao ya wajasiriamali kutoka maeneo tofauti kulingana na mahitaji.

No comments:

Post a Comment