Wednesday, May 16, 2012

KIFAA CHA KUPIMIA "NGOMA"

Jopo la wanasayansi nchini Marekani limependekeza kuidhinishwa kwa kifaa cha kupima virusi vya ukimwi kwa matumizi ya nyumbani.
Kifaa hicho kwa jina OraQuick, kinatumia mswaki kutambua chembechembe za virusi kwenye mate katika kipindi cha dakika ishirini.
Ikiwa kifaa hicho kitaidhinishwa na idara ya ukaguzi wa dawa na chakula, kitakuwa cha kwanza kuuzwa kwenye maduka ya dawa kwa matumizi ya nyumbani.
Baadhi ya wanajopo wanamesema kuwa kifaa hicho kinafaa kuwekwa maandishi ya kuonya kuwa huenda matokeo ya vipimo vyake yasiwe ya kweli kwani hakifanyi kazi kwa uhakika wa asilimia mia moja.

No comments:

Post a Comment