Wednesday, May 16, 2012

Ratko Mladic mahakamani

Kamanda wa zamani wa jeshi la Bosnia Ratko Mladic alikuwa na nia "ya kuangamiza jamii fulani" Bosnia,hayo yalifahamika katika siku ya kwanza ya kesi yake ya uhalifu wa kivita.
Jenerali Mladic anakabiliwa na mashtaka 11 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mauaji ya kimbari, kuhusiana na mauaji mabaya ya mwaka 1992-95 wakati wa vita vya Bosnia.
Viongozi wa mashtaka katika mahakama ya The Hague wanasema wataonyesha kuhusika kwake katika uhalifu huo.
Ametaja shutuma hizo kama "unyama" na mahakama imesema kwa niaba yake kuwa kwa sasa hana hatia.
Jenerali Mladic anashutumiwa kupanga mauaji ya vijana na wanaume wa kiislamu 7,000 Srebrenica mwaka 1995.
Pia ameshtakiwa kwa kuhusika na mashambulio ya miezi 44 ya Sarajevo wakati huo watu zaidi ya 10,000 waliuawa.

No comments:

Post a Comment