Thursday, December 1, 2011

REDONDO VS AZAM FC

KIUNGO wa Azam Fc Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema hana taarifa za kupelekwa kwa mkopo timu ya Moro United.
"Mimi nasikia kwenye vyombo vya habari kwamba natakiwa kwenda kwa mkopo Moro United. Sina taarifa kutoka timu yangu, isitoshe hata kama ni kweli, sina mpango wa kwenda huko," alisema Redondo.
Redondo aliyesajiliwa Azam akitoka Simba, ameulalamikia utaratibu uliotumiwa na Azam kwa vile umefanyika kimya kimya na haukuonyesha kumthamini.
"Mimi najiamini, uwezo wa kucheza ninao na naweza kuuzika kwa timu yoyote," alisema Redondo.
Amesema ameshtushwa na taarifa hizo na kama sababu ya kumtoa kwa mkopo ipo, basi ni vizuri wangempa kwanza taarifa kama taratibu za kuwatoa wachezaji kwa mkopo zinavyoeleza

No comments:

Post a Comment