Monday, December 19, 2011

Dhoruba ya Philippines yauwa wengi

Watu zaidi ya 800 bado wametoweka nchini Philippines baada ya kimbunga kilichosomba vijiji kusini mwa nchi, katika kisiwa cha Mindanao.
Maelfu ya wanajeshi wanashiriki katika shughuli za uokozi, na bado wameshindwa kufikia vijiji vya mbali ambavyo vimefunikwa na mafuriko na maji ya pwani yaliyojaa.
Imethibitishwa kuwa watu zaidi ya 650 wamekufa.
Wakuu wamelaumiwa kwa kutowaonya watu mapema, kwamba dhoruba inakaribia.
Eneo hilo liko kusini zaidi ya yale yanayokumbwa mara nyingi na vimbunga kila mwaka nchini Philippines.

No comments:

Post a Comment