Thursday, December 29, 2011

ASKARI ASHEREKEA KRIMAS KWA KICHAPO

Wakati wakristo hapa nchini wameungana na wakristo kote ulimwenguni katika kusherekea siku ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo ,askari mmoja wa kituo cha polisi Mafinga wilaya ya Mufindi amejikuta akisherekea vibaya sikukuu hiyo baada ya kuvamiwa na watu wasiofahamika na kujeruhiwa kwa mapanga .

Tukio hilo limetokea eneo la Kinyanambo katika mji wa Mafinga na wapasha habari wa mtandao huu wa
www.habarizamitaa.blogspot.com kufikisha taarifa hizo kuwa askari huyo alikutwa akiwa amepigwa vibaya na kuumizwa katika eneo hilo na kukutwa yu hoi bini tabani majira ya saa 7 za usiku.

Taarifa hizo zimethibitishwa pia na mmoja kati ya askari wa kituo cha polisi Mafinga ambaye amedai kuwa pona ya askari huyo ilitokana na askari mwenzao ambaye ni dereva wa gari la OCD Mafinga kufika na kumsaidia kumkimbiza hospital kwa matibabu na sasa bado anaendelea kutibiwa japo ni nje ya Hospital hiyo ya Mafinga.

Hadi sasa chanzo cha tukio hilo bado kutajwa japo baadhi wanahusisha tukio hilo la masuala ya kimapenzi na kuwa yawezekana afande huyo alikuwa katika mawindo ya kusaka kimwana wa kusherekea nae siku kuu hiyo.

No comments:

Post a Comment