WANANCHI wenye hasira kali wakazi wa Kigamboni kata ya Mwangata katika
manispaa ya Iringa nusuru wamuue kwa kichapo kijana mmoja anayetuhumiwa
kuwa ni mmoja kati ya watuhumiwa wa upigaji nondo katika eneo hilo.
Mtuhumiwa
huyo anadaiwa kuwa ni mmoja kati ya vijana wa jambazi sugu ambalo
linaendelea kutafutwa katika eneo hilo Msafiri Ilomo ambaye alipata
kukutwa na mali mbali mbali zinazodaiwa kuwa ni mali ya wizi zaidi ya
Lori moja katika nyumba yake iliyovunjwa na kuchomwa moto baada ya
serikali kuamuli ibomolewe.
Wakielezea juu ya tukio hikio hilo wakati wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com
wakazi wa eneo hilo akiwemo diwani wao Galus Lugenge walisema kuwa
kijana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kutokana na zoezi
linaloendelea la kusaka wahusika wote wa mtandao huo ambao wametajwa na
mtuhumiwa huyo kabla ya kupigwa na kupoteza fahamu usiku wa leo.
Hata
hivyo walisema kuwa zoezi la kuwasaka wahusika zaidi wa tukio hilo bado
linaendeklea na kufanywa na wananchi wa kata hiyo hasa wakazi wa
Kigamboni.
No comments:
Post a Comment