UNANINI EWE ULALAYE USINGIZI?
Nchi yetu inapita katika vipindi mbalimbali
vigumu na ambavyo hatukuwahi kuvipitia kabla. Chuki imeongezeka kwa kiwango cha
ajabu na watu huchekeana tu kwasababu ya MAZOEA TU. upendo wa kweli unafifia
kimya na GIZA LA MACHAFUKO NA MATENGANO linaingia huku wengine wakishangilia kana kwamba ndio
kunapapmbazuka na tumaini jipya.
NINANI MWENYE JUKUMU?
UKISOMA KATIKA KITABU CHA YONA 1:1-4
Utaona YONA anatumwa kwenda kufanya kazi
katika mji mmoja na YEYE KWA UKAIDI anaamua kwenda alipo taka yeye. Katika hali
ile ya kulazimisha aende atakako akajikuta kawaingiza na wengine matatani bila
kujijua.
Chombo alichopanda ili ajiepushe na USO (KUSUDI)
WA BWANA MUNGU KIKAPIGWA NA DHORUBA KALI
kiwango ambacho kilizua hofu kwa waliomo katika chombo. Ikawa kila mtu
akijaribu kumkumbuka na kumwomba MUNGU WAKE ili mambo ya tulie lakini aliye
watumbukiza wengine kwenye kadhia hio alikua amelala
YONA 1:
4 Lakini Bwana
alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa
karibu na kuvunjika.
5 Basi
wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini
shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa
ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi.
6 Basi
nahodha akamwendea, akamwambia, UNA NINI, EWE ULALAYE USINGIZI? AMKA, UKAMWOMBE
MUNGU WAKO; LABDA MUNGU HUYO ATATUKUMBUKA, TUSIPOTEE.
KWAHIO
Yona 1: 11 Basi wakamwambia,
Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka.
12 Naye akawaambia, NIKAMATENI,
MNITUPE BAHARINI; BASI BAHARI ITATULIA; KWA MAANA NAJUA YA KUWA NI KWA AJILI
YANGU TUFANI HII IMEWAPATA.
13 Lakini wale watu
wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari
ilizidi kuwachafukia sana.
au
LUKA 21: 34 Basi,
jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya
maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo
itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36 BASI, KESHENI
NINYI KILA WAKATI, MKIOMBA, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea,
na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
Mimi na wewe tunaweza tukaamua kusimama katika nafasi zetu
na kuamua kumuomba mungu atusaidie kwa ajili
ya nchi hii ili tusiingie katika machafuko na chuki kuu. Tuombe kwa moyo wa
dhati kwaajili ya nchi yetu ili:-
-ISIINGIE KATIKA CHUKI ZA KIDINI NA KISIASA
-ISIINGIE KATIKA VITA NAN CHI JIRANI
-ISIINGIE KATIKA MIKATABA YA KINYONYAJI
-ISIINGIE KATIKA MIKATABA YA KISHOGA NA KISAGAJI NA YOTE
YALIO CHUKIZO MACHONI PA MUNGU.
LAKINI KUMBUKA MAOMBI HAYA YOTE YANAANZA NA WEWE SIO LAZIMA
YAANZE NA KIONGOZI WAKO WA KIDINI ILA UNAWEZA KUMSHAURI TU KAMA ATAONA NI VEMA
ASHIRIKISHE NA JUMUIA KUBWA YA WATU
WARAKA WANGU KWA WAPENDWA WOTE
MARKO MANGARA MATHIAS
No comments:
Post a Comment