Katika mikutano mbalimbali ya kiroho ambayo kwa rehema za
MUNGU nilifanikiwa kuhudhuria nimekua nikiona wara ifikapo saa ya MAOMBEZI
idadi ya wanaoanguka kati ya WANAUME na WANAWAKE, idadi kubwa ya watakao anguka
ni WANAWAKE.
SWALI KWANINI WANAWAKE?
1.-KUIANGUSHA JAMII
Kwanza tuanze kutazama historia kuanzia kwa “MAMA YETU
EVA/HAWA” tukisoma kitabu cha MWANZO 3 tutaona namna ambavyo shetani na
mwanamke wakiwa katika mazungumzo ambayo mwisho wa “mazungumzo” yale nyoka
anafanikiwa kumhadaa na mwanamke anakula TUNDA NA ANAMWEKEA NA MUMEWAKE ambapo
baadae tunakuja kuambiwa ndio mwanzo wa ANGUKO LA MWANADAMU.
--huu ni ushahidiwa namna ambavyo ADUI ANAWEZA KUMTUMIA
MWANAMKE KUISHAMBULIA JAMII
2.KUIINUA JAMII
Ukikisoma vizuri kitabu cha ESTA (ambaye ni mwanamke) utaona
namna ambavyo MUNGU alivyo mtumia mwanamke KUWAOKOA WATU WAKE NA UDHALIMU WA
HAMANI na mwisho hamani akafa na WATU WA MUNGU WAKAPATA UKOMBOZI.
KWANINI MWANAMKE?
Ukisoma kitabu cha UFUNUO 12 utaona shetani /joka akijaribu
kupambana na MWANAMKE na UZAO WAKE. UFUNUO 12: 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao
wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye
akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Ukisoma UFUNUO 12 yote
utaona hadithi kamili ya namna ilivyo kuwa
JIBU: MWANAMKE ni mshirika
wa KARIBU NA WA MUHIMU SANA katika ulimwengu kwasababu ndipo uzao/ uzazi
hutunzwa kwa MWANAMKE kwa njia ya mimba. Na kitaalam MIMBA ilioko tumboni mwa
MWANAMKE huwa na muunganiko wa mojakwa moja kwa njia ya DAMU muunganiko ambao
hauepukiki. Hivyo basi kupitia kwa mwanamke VIBAYA NA VYEMA HUPITA HAPO.
Hivyo shetani anawashambulia
sana WANAWAKE KWA MAANA AKIFANIKIWA KUWAPATA NA KUWAHARIBU (DESTRUCT) WANAWAKE
tayari atakua ameuharibu ULIMWENGU.
THEME:
WANUME TUWALINDE WANAWAKE
kwa MAOMBI na malezi mema ili shetani asipate nafasi katika maisha yao ILI
ISIWE CHANZO CHA UHARIBIFU.
WANAWAKE
WEWE NI CHOMBO MUHIMU KATIKA
ULIMWENGU WA ROHO NA MWILI HIVYO
Mjilinde na kila lisiliojema
MAANA MNADHAMANA YA KUUZAA ULIMWENGU NA
KUUFANYA SEHEMU SALAMA
MUNGU AWABARIKI, AWALINDE NA
KUWAONGOZA WANAWAKE ILI SHETANI ASIPATE NAFASI KATIKA ULIMWENGU NA FAMILIA ZETU
NA JAMII ZETU.
MARKO MANGARA MATHIAS
No comments:
Post a Comment