ZAIDI YA WATU 30 WAUWAWA KATIKA MAKABILIANO KATI YA POLISI NA WACHIMBA
MIGODI WANAOGOMA AFRIKA KUSINI.
WAZIRI WA POLISI WA
AFRIKA KUSINI AMESEMA MAAFA HAYO YALITOKEA SIKU YA ALHAMISI KATIKA MGODI WA
MARIKANA.
POLISI WALIFYATUA
RISASI BAADA YA KUSHINDWA KUWATAWANYA WAGOMAJI HAO WALIOKUWA WAMEJIHAMI KWA
MARUNGU NA MAPANGA.
MGODI HUO WA DHAHABU
NYEUPE UNAOMILIKIWA NA KAMPUNI YA LONMIN IMEKUWA NI SEHEMU YA MAPIGANO MAKALI
KUHUSU MZOZO WA MALIPO ULIOTOKANA NA UHASAMA KATI YA VYAMA VIWILI VYA
WAFANYAKAZI.
KISA HICHO CHA POLISI
NI MOJA WAPO WA OPERESHENI MBAYA ZAIDI YA POLISI TANGU KUMALIZIKA KWA ENZI ZA
UBAGUZI WA RANGI.
AWALI MACHAFUKO HAYO
YALIOANZA WIKI ILIYOPITA YALIKUWA YAMESABABISHA VIFO VYA WATU 10 NA POLISI
WAWILI.
SIKU YA IJUMAA WAZIRI
WA POLISI ,NATHI MTHETHWA AKIZUNGUMZA NA KITUO KIMOJA CHA RADIO ALITHIBITISHA
KUWA WATU WENGI WALIJERUHIWA NA WENGINE KUUWAWA.
CHAMA KIKUU CHA
WACHIMBA MIGODI, NATIONAL UNION OF MINEWORKERS ,KINASEMA IDADI YA WALIOFARIKI
NI 36.
POLISI WALIKUWA
WAMEPELEKWA KWENDA KUWATAWANYA WACHIMBA MIGODI WAPATAO 3,000 AMBAO WALIKUWA
WAMEKUSANYIKA ENEO LA MLIMA MKABALA NA MGODI WA MARIKANA, AMBAO UKO KILOMITA
100 KASKAZINI MANGHARIBI MWA JOHANNESBURG.
WAFANYAKZI HAO
WALIKUWA WANATAKA NYONGEZA YA MSHAHARA YA DOLA $1,000 KILA MWEZI.
MAZINGIRA YALIOFANYA
POLISI WAANZE KUFYATUA RISASI BADO HAIJAJULIKANA , LAKINI TAARIFA KUTOKA KWA
WALIOSHUHUDIA ZINASEMA MAUJI HAYO YALITOKEA WAKATI KUNDI LA WAANDAMANI
WALIPOJARIBU KUWAVAMIA POLISI.
HAPO NDIPO POLISI
WALIOKUWA WAMEJIHAMI KWA BUNDUKI NA BASTOLA WAKAANZA KUFYATUA RISASI.
No comments:
Post a Comment