VURUGU KUBWA
ZIMEIBUKA JUZI KATIKA MBEZI JUU, WILAYA YA KINONDONI, DAR ES SALAAM BAADA YA
KUNDI LA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU, KUWAVAMIA NA KUWASHAMBULIA WAUMINI WA
KANISA LA SALVATION MINISTRY FOR ALL NATION (SMAN), LILILOPO ENEO HILO NA
KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI.
INADAIWA
KUWA, MALI ZILIZOHARIBIWA ZINA THAMANI YA ZAIDI YA SH. MILIONI SITA AMBAPO
CHANZO CHA VURUGU HIZO NI MGOGORO ULIOANZA TANGU DESEMBA 2011.
AKIZUNGUMZA
NA MAJIRA, MCHUNGAJI WA KANISA HILO FRED MWAMTEMA (48), ALIDAI UVAMIZI HUO
UMEFANYIKA ZAIDI YA MARA NNE NA KUHARIBU MALI ZA KANISA KWA MADAI YA KUPIGIWA
KELELE WANAPOKUWA KATIKA IBADA ZAO KARIBU NA KANISA HILO.
ALISEMA
WAUMINI WA KIISLAMU WALIOFANYA VURUGU HIZO NI WALE WANAOSALI KATIKA MSIKITI WA
AL MUBARAK MASJID ULIOPO JIRANI NA KANISA LAO KATIKA KATA YA NDUMBWI.
“MGOGORO HUO
ULIANZA MUDA MREFU, WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WALISHAKUJA MARA KADHAA NA
KUDAI WANASHINDWA KUFANYA IBADA KUTOKANA NA KELELE ZINAZOTOKA KANISA,” ALISEMA.
ALIONGEZA
KUWA KUTOKAANA NA HALI HIYO, VIONGOZI WA MSIKITI HUO WALIOAMUA KUWASHTAKI KWA
OFISA MTENDAJI WA KATA HIYO LAKINI HAKUNA MUAFAKA ULIOWEZA KUPATIKANA.
MCHUNGAJI
MWAMTEMA ALISEMA AGOSTI 12 MWAKA HUU, WAKIWA KWENYE IBADA, GHAFLA WALIVAMIA NA
KUNDI LA WAISLAMU, KUWAPIGA WAUMINI NA KUHARIBU MALI ZA KANISA KAMA VITI,
VYOMBO VYA MUZIKI, MATURUBAI, KUCHOMA MOTO KAPETI NA KUNG'OA NYAYA ZA UMEME.
“TUNAOMBA
VYOMBO VYA DOLA VIINGILIE KATI MGOGORO HUU ILI UWEZE KUPATIWA UFUMBUZI WA
HARAKA KWANI UNAWEZA KUSABABISHA MADHARA KAMA HATUA HAZITACHUKULIWA,” ALISEMA.
ALISEMA
UONGOZI WA KANISA HILO ULIAMUA KUTOA TAARIFA KITUO CHA POLISI CHA KAWE AMBAPO
WAUMINI WA DINI HIZO, WALITAKIWA KUACHA KUFANYIANA FUJO NA KILA MMOJA AHESHIMU
DINI YA MWENZAKE.
PAMOJA
POLISI KUTOA AGIZO HILO, INADAIWA WAUMINI WA KIISLAMU WALIVAMIA TENA KANISA
HILO AGOSTI 15 MWAKA HUU, WAKATI WA MKESHA NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI.
JUHUDI ZA
GAZETI HILI KUWAPATA VIONGOZI WA MSIKITI HUO ZILISHINDIKANA LAKINI MUUMINI
MMOJA AMBAYE HAKUTAKA JINA LAKE LIANDIKWE GAZETINI, ALISEMA WAISLAMU NDIO
WALIKUWA WA KWANZA KUJENGA MSIKITI KATIKA ENEO HILO.
“BAADA YA
MUDA TUKAONA WENZETU NAO WANAJENGA KANISA NA KUPIGA KELELE WAKITUMIA
MATARUMBETA WAKATI WAISLAMU WAKIWA KWENYE IBADA ZAO HIVYO KUSABABISHA MGOGORO
HUU KUENDELEA,” ALISEMA.
AKITHIBITISHIA
KUTOKA KWA VURUGU HIZO, KAIMU KAMANDA MKOA WA KIPOLISI KINONDONI, JOHN
MTALIMBO, ALISEMA MGOGORO HUO UMEDUMU MUDA MREFU BILA MUAFAKA KUPATIKANA.
“MTOA
TAARIFA MCHUNGAJI MWAMTEMA AMBAYE NDIYE KIONGOZI WA KANISA HILI ALIDA WAUMINI
WA KIISLAMU WANAWAFANYIA VURUGU AMBAPO KUNDI LA WATU 30 AKIWEMO SHEKHE WA
MSIKITI HUU ABDU SWEDI (41), MKAZI WA MBEZI JUU, WALIVAMIA KATIKA KANISA HILO
NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI,” ALISEMA.
ALISEMA
KUTOKANA NA HALI HIYO, MCHUNGAJI MWINGINE WA KANISA HILI ELIA SUDI (32), MKAZI
WA MWANANYAMALA, ALIJERUHIWA VIBAYA KICHWANI KWA KUPIGWA NA KITU CHENYE NCHA
KALI.
KAMANDA
MTALIMBO ALISEMA VURUGU HIZO ZILISABABISHA UHARIBIFU WA VITI 25 VYA PLASTIKI,
VIPAZA SAUTI VINNE NA KUIBWA KWA KAMERA AINA YA SANYO AMBAPO JESHI HILO
LINAMSHIKILIA SHEKHE SWEDI.
No comments:
Post a Comment