WIZARA YA
MALIASILI NA UTALII IMECHUKUA HATUA ZA KINIDHAMU KWA WATUMISHI WAKE TISA (9)
KUFUATIA KADHIA YA UTOROSHAJI WA WANYAMAPORI HAI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA
WA KILIMANJARO (KIA) NA MASUALA MENGINE YANAYOHUSU WANYAMAPORI. WATUMISHI HAO
WAMECHUKULIWA HATUA HUSIKA KUFUATIA KUKAMILIKA KWA UCHUNGUZI WA TUHUMA
ZILIZOKUWA ZIKIWAKABIRI.
(1)
WALIOFUKUZWA KAZI KUTOKANA NA UKIUKAJI WA SHERIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU
YAO NI:
- BW. OBEID
F. MBANGWA - MKURUGENZI WA WANYAMAPORI. WAKATI WA KADHIA HIYO ALIKUWA
MKURUGENZI MSAIDIZI MATUMIZI YA WANYAMAPORI,
- BW. SIMON
CHARLES GWERA – OFISI YA UWINDAJI WA KITALII – CITES NA UTALII WA PICHA ARUSHA,
- BW FRANK
MREMI - OFISI YA UWINDAJI WA KITALII – CITES NA UTALII WA PICHA ARUSHA.
(2)
ALIYEONDOLEWA CHEO CHA MADARAKA KUTOKANA NA KUTOCHUKUA HATUA KAMILIFU ZA ULINZI
AMBAZO ZINGEWEZA KUZUIA KUTOKEA KWA TUKIO LA UTOROSHWAJI WA WANYAMA NI:
- BW.
BONAVENTURA M.C. MIDALA – MKURUGENZI MSAIDIZI, UNDELEZAJI WANYAMAPORI. WAKATI
WA TUKIO ALIKUWA MKURUGENZI MSAIDIZI SEHEMU YA KUZUIA UJANGILI.
(3) WAFUATAO
NI MAAFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II WALIOTEKELEZA MAELEKEZO YA WAKUU WAO WA
KAZI YALIYO KINYUME CHA SHERIA AMBAO WAMEPEWA ONYO KALI LA MAANDISHI:
- BIBI
MARTHA P. MSEMO - AFISA LESENI, OFISI YA UWINDAJI WA KITALII, CITES NA UTALII
WA PICHA ARUSHA.
- BIBI
ANTHONIA ANTHONY – AFISA LESENI, OFISI YA UWINDAJI WA KITALII, CITES NA UTALII
WA PICHA DAR ES SALAAM.
(4) BW.
SILVANUS ATETE OKUDO NI MKUU WA KITUO CHA UWINDAJI WA KITALII, CITES NA UTALII
WA PICHA ARUSHA ALIYESHINDWA KUFUATILIA KUPATA MAELEKEZO YA MKURUNGEZI WA
WANYAMAPORI KUHUSU MTUMISHI WAKE ALIYEKIUKA SHERIA KATIKA UTOAJI WA VIBALI.
AIDHA, ALISHINDWA KUPELEKA KWA KATIBU MKUU TAARIFA KUHUSU MTUMISHI HUYO ILI
ACHUKULIWE HATUA ZA NIDHAMU.
- SILVANUS
ATETE OKUDO – AMEPEWA ONYO KALI LA MAANDISHI.
(5) WAFUATAO
NI MAAFISA AMBAO UCHUNGUZI DHIDI YAO UNAENDELEA:
- BW.
MOHAMED MADEHELE – OFISI YA MATUMIZI ENDELEVU YA WANYAMAPORI
- BIBI
MARIAM NYALLU – KITUO CHA UWINDAJI WA KITALII, CITES NA UTALII WA PICHA –
ARUSHA.
WAHUSIKA
WENGINE KATIKA KADHIA HIYO WASIOKUWA WAAJIRIWA WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
WATACHUKILIWA HATUA NA MAMLAKA NYINGINE HUSIKA.
MHE. KHAMIS
SUEDI KAGASHEKI
WAZIRI WA
MALIASILI NA UTALII
13 AGOSTI
2012
(IMETOLEWA
KWENYE PRESS CONFERENCE ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE DODOMA TAREHE 13
AGOSTI 2012).
No comments:
Post a Comment