Wednesday, October 23, 2013

MGOMO WA VYOMBO VYA MOTO VYA MIZIGOBen Komba/Pwani-Tanzania/21-10-2013/13;30

Madereva wa Magari madogo ya mizigo,na Pikipiki aina ya Toyo na Bajaj wamefanya maandamano ya amani kuelekea ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha kushinikiza kuwekewa kwa miundombinu katika eneo ambalo wanafanya shughuli zao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi akizungumza na mmoja wa Viongozi wao, BW.ABDALLAH ZANDA amesema kitu kikubwa kilichowafanya wachukue hatua ya kuandamana ni Polisi kuwakamata wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku.

BW.ZANDA amebainisha kwa kipindi kirefu halmashauri walitoa agizo la magari na pikipiki za kubeba mizigo kuhama eneo hilo, jambo ambalo wao kwa upande wao hawana kipingamizi nalo, lakini tatizo ni kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika katika eneo hilo.

Amefafanua baadhi ya vitu muhimu ambavyo vinakosekana ni pamoja na huduma ya choo katika sehemu ambayo inakaa karibu watu 100, mabanda ya mamalishe, kukosekana kwa mabanda ya kupumzikia madereva na wateja na hivyo kuonekana halmashauri kama imekurupuka kuanzisha zoezi hilo.

Ofisa mipango halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. JOHNSON NYAMITI amewataka madereva wa magari madogo ya mizigo na pikipiki hao kuwa watulivu na ameshukuru kukutana nao na kuwaahidi yale ambayo yoyote wameyalalamikia yatapatiwa ufumbuzi.

BW. NYAMITI amewaasa madereva kuwekwa kwao pale wasjichukulie kama wametelekezwa bali halmashauri inafahamu uwepo wao na itahakikisha inaweka kifusi eneo hilo ili liweze kutumika kipindi chote cha Mwaka.

No comments:

Post a Comment