Monday, September 16, 2013

CHADEMA KUZINDUA OPERESHENI ZINDUKA KIBAHA.



Ben Komba/Pwani-Tanzania/13-09-2013/03:39

Chama cha Demokrasia na maendeleo mjini Kibaha mkoa wa Pwani wameanzisha mpango mkakati maalum wa kutembelea mitaa, katika operesheni itayokwenda na jina la ZINDUKA.

Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani Kibaha, BW.BUMIJA SENKONDO amesema msukumo wameupata kutokana na kushuhudia ushirikishwaji mdogo wa wananchi katika maamuzi muhimu yanayowahusu na hivyo watatumia opersheni hiyo kuwazindua wananchi juu ya mambo yanayofanywa na chama tawala.

BW.BUMIJA amebainisha kuwa katika Bajeti ya halmashauri ya mji wa Kibaha asilimia 90 ya miradi iliyotekelezwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 haikuwahusisha wananchi katika uibuaji wa miradi kulingana na mahitaji yao kama inavyoelekezwa na sheria za serikali za mitaa.

Mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, BW.BUMIJA SENKONDO amefafanua kuwa operesheni hiyo itaenda sambamba na kupokea wanachama wapya na kujenga uhai wa Chama.

Aidha ameongeza kuwa operesheni hiyo itafanyika katika awamu nne ambapo Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa, BW.WILBROAD SLAA anatarajiwa kufunga awamu hiyo ya operesheni kunako SEPTEMBA 29 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment