Sunday, August 18, 2013

ADAM UKOWAPI WEWE?

ADAM UKOWAPI WEWE?



MWANZO 3: 9  Bwana MUNGU akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
Sote tunajua yakuwa MUNGU anauwezo wa kutuona popote tulipo iwe juu ya dari, kichakani, chumbani ma sehemu yoyote ile. Lakin ni vema tuka jiuliza swali hili ni kwanini MUNGU alimuuliza Adam swali hili MWANZO 3: 9  BWANA MUNGU AKAMWITA ADAMU, AKAMWAMBIA, UKO WAPI?
Je , ni nini kilitokea?
Ukisoma kitabu cha mwanzo 3 utaona kulikua na mazungumzo ya nyoka (shetani) na mwanamke ambapo matokeo yake ni wengi tunayajua na inasadikiwa yametuathiri hadi leo hii. Lakin ukweli ni kuwa katika hali ya kawaida kumshawishi mwanamke ili afanye jambo lolote ambalo hakulipanga inahitaji muda mrefu ili aweze kulielewa na kulifanya hivyo katika hali ya kawaida inawezekana ilimchukua nyoka (shetani) muda mrefu pengine siku kadhaa akijaribu kumshawishi mwanamke hadi akafanikiwa  lakin katika muda wote huo hatukuambiwa adam alikuwa wapi? Ukisoma MWANZO 2:18  Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Kwa maana watakuwa wana saidiana katika mambo mbalimbali hivyo popote alipo Adam alitakiwa aidha mkewe awepo au ajjue alipo mumewe, halikadhalika na Adam alitakiwa ajue alipo mkewe muda na saa yoyote. Je  ni kitu gani kilitokea hadi Adam hakujulikana alipo na mkewe akadanganywa na shetani?
Je nani alaumiwe?
Je tumlaumu mwanamke kwa kukubali kukaa kitako na kuongea na shetani (nyoka) kwa muda wote wa mazungumzo yao bila kumshirikisha mumewe?
Au
Tumlaumu Adam ambaye yeye alipewa maelekezo na MUNGU na kukabidhiwa mwanamke ili amlinde na yeye akashika mambo mengine na kuacha KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKE

Kwa leo tumlaumu Adam kwamaana kama ingekua amesimama vyema katika nafasi yake  basi shetani asingelipata nafasi ya kukaa na kumshawishi mke wa Adam. Lakin pia baada ya nyoka kumrubuni Hawa ilipaswa Adam kama kiongozi akatae kulila lile tunda kutokusimama katika nafasi yake pia yeye kama kiongozi alipaswa asijifiche lakin arudi mbele za MUNGU kwaajili ya TOBA ili kusawazisha mambo yake na MUNGU.

THEME
Sisi kama binadamu MUNGU ametuita katika nafasi mbalimbali na tofauti tofauti ilituyatimize malengo mbalimbali ambayo ndio makusudi ya uwepo wetu hapa duniani lakini sisi tumekua “BUSY” na mambo mengine yanayotupendeza machoni petu hatakama ni kinyume na kusudi la MUNGU.
HIVYO
KWAKUWA UWEPO WAKO NI SULUHISHO LA JAMBO FULANI KATIKA MAISHA HAYA SIMAMA KATIKA NAFASI YAKO ILI ULITATUE JAMBO KATIKA JAMII YAKO.
IKIWA
Ikiwa hujui kusudi la kuishi kwako ulimwenguni rudi katika sala kwa kuomba ikibidi kufunga ili KUSUDI LA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO LITIMIE.
MUNGU ANASEMA.
1 WAKORINTHO 2: 8  lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
9  Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

WARAKA WANGU KWA WAPENDWA WOTE (N0 3)

MARKO MANGARA MATHIAS

No comments:

Post a Comment