Sunday, June 9, 2013

SUMATRA WAAMKA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/06/2013/13:32 Watanzania wametakiwa kutoa ushirikiano stahili kwa SUMATRA wanapokuwa safarini ili kuweza kupunguziwa kero zinazowapata wanapokuwa wanasafiri kuelekea maeneo mbalimbali ya Tanzania. Afisa mfawidhi mkuu wa SUMATRA mkoa wa Pwani, BW.NASHON IROGA amesema hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kufuatia uwepo wa kampeni maalumu ya ukaguzi wa mabasi inayoendeshwa katika kituo kikuu cha mabasi mjini Kibaha. BW.IROGA amebainisha kuwa operesheni hiyo inayoendeshwa sambamba na askari wa usalama barabarani, na lengo kubwa la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanadhibiti vitendo vyote vya mabasi ya abiria kukatisha ruti,kutototoa tiketi kwa abiria na mengine. Amefafafanua kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazojitokeza ambazo nyingi zinasababishwa na madereva kukiuka taratibu za usafirishaji kwa makusudi kutokana na kuzongwa na tama, akitoa mfano wa mabasi yanayofanya safari za Ubungo mpaka Mlandizi, ambayo nyakati za jioni yanaishia Mbezi kutokana na abiria wa Mbezi kuwa tayari kulipa nauli y ash.1000/= ambayo ni nauli ya Ubungo-Mailimoja. Afisa huyo mfawidhi wa SUMATRA mkoa wa Pwani, BW. NASHON IROGA ameongeza kuanzia sasa mtu yoyote ambaye atakatisha ruti atachukuliwa hatua stahili za kisheria ikiwa pamoja na kufuatiwa leseni na amewaasa wananchi kutokuwa na ghadhabu wakati wao wanatekeleza wajibu wao.

1 comment:

  1. My brother recommended I might like this blog. He was totally right.
    This post actually made my day. You can not imagine
    simply how much time I had spent for this info! Thanks!


    my web site - shanghai masters golf final leaderboard

    ReplyDelete