Friday, February 22, 2013

FULL COUNCIL KIBAHA TC



BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/21-FEB-13/18:38:58

KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2012/2013 HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA IMEFANIKIWA KUTEKELEZA NA KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA KATIKA KWA UFANISI MKUBWA KATIKA MAENEO MBALIMBALI IKIWEMO AFYA,USAFI WA MAZINGIRA, ELIMU NA UIMARISHAJI WA MIUNDO MBINU YA BARABARA IKIWA PAMOJA NA KUNUNUA GREDA.

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA, BI.JENIFA OMOLO AMEBAINISHA KUWA HALAMSHAURI YAKE KATIKA KIPINDI CHA FEDHA KINACHOISHIA JULAI MWAKA HUU, ILIKADIRIA KUKUSANYA SHILINGI BILIONI 18 LAKINI MPAKA SASA KIASI KILICHOKUSANYWA NI SHILINGI BILIONI NANE TU, NA JUHUDI ZINAFANYIKA KATIKA KUHAKIKISHA LENGO HILO LINAFIKIWA AU KUVUKWA KWA KUBUNI VYANZO MBALIMBALI VYA KUJIKUSANYIA MAPATO.

BI.OMOLO AMEONGEZA KUWA HALMASHAURI YAKE IMELENGA KUKUSANYA MAPATO HAYO KATIKA VYANZO MBALIMBALI IKIWEMOMAEGESHO YA MAGARI, MACHIMBO YA MCHANGA, KODI ZA MAJENGO, KODI YA ARDHI NA MSURUR WA KODI NYINGINE MBALIMBALI KAMA ILIVYOAINISHWA KATIKA HOTUBA YA BAJETI YA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA MWAKA 2012/2013.

AKICHANGIA MAPENDEKEZO NA MAKADIRIO YA BAJETI YA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA, MKUU WA WILAYA YA KIBAHA, BIBVI. HALIMA KIHEMBA AMESEMA JAMBO JEMA KWA BAJETI NI UTEKELEZAJI WA MIPANGO KWA KADIRI YA ILIVYOKUSUDIWA KATIKA HOTUBA YA BAJETI YA BAJETI KATIKA KIKAO MAALUM CHA BARAZA LA MADIWANI IULI KUFIKIA MALENGO NA KUPIGA HATUA KIUTENDAJI.

KATIKA HATUA NYINGINE MKUU WA WILAYA YA KIBAHA, BIBI. HALIMA KIHEMBA AMEWAHIMIZA MADIWANI KUCHUKUA HATUA ZA MAKUSUDI ZA KUIMARISHA HALI YA ULINZI NA USALAMA KATIKA MAENEO YAO NA HASA KUTOKANA NA KUPANUKA KWA MJI NA KUHAMIA KWA WATU KUTOKA MAENEO TOFAUTI, NA HIVYO KUWATAKA MADIWANI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA KATA WANALISIMAMIA SUALA HILI KWA UMAKINI MKUBWA KATIKA KUEPUSHA KUIPA MZIGO KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA.

1 comment: