Sunday, January 13, 2013

ZITTO AKALIA KUTI KAVU


MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI, ZITTO KABWE AMEINGIA MATATANI, BAADA YA KUTAKIWA KUKANUSHA TUHUMA ALIZOZITOA BUNGENI KATIKA MKUTANO WA TISA WA BUNGE, KWAMBA MFANYABIASHARA WA KIGENI, MOTO MABANGA, ALIPEWA VITALU VYA MAFUTA KINYUME NA TARATIBU.
MFANYABIASHARA HUYO AMESEMA KUWA IWAPO ZITTO ATASHINDWA KUKANUSHA TUHUMA HIZO, ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
BARUA ILIYOANDIKWA KWENDA KWA MBUNGE HUYO ILIYOSAINIWA NA MWANASHERIA WA MABANGA, LAWLEY SHEIN WA KAMPUNI YA UWAKILI YA LAWLEY SHEIN ATTORNEYS, AMBAYO MWANANCHI JUMAPILI LIMEIONA, INAELEZA KUWA HOJA BINAFSI ALIYOITOA ZITTO, HAIKUWA NA UKWELI WOWOTE.
BARUA HIYO YA TAREHE 28 NOVEMBA, 2012 ILISEMA KUWA HOJA HIYO YA ZITTO NI YA UONGO, IMEMKASHIFU MTEJA WAO NA KUMSHUSHIA HADHI YAKE BINAFSI NA BIASHARA ZAKE.

No comments:

Post a Comment