Tuesday, January 8, 2013

MESSI BORA KWA MARA YA NNEAMBWAGA RONALDO.MSHAMBULIAJI WA BARCELONA NA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA LIONEL MESSI AMESHINDA TUZO YA BALLON D'OR KWA MWAKA WA NNE MFULULIZO.

MESSI, 25, ALIFUNGA JUMLA YA MAGOLI 91 MWAKA WA 2012 NA ALIWASHINDA WACHEZAJI WENGINE ANDRES INIESTA WA BARCELONA NA CHRISTIANO RONALDO WA REAL MADRID.

LICHA YA KUFUNGA IDADI HIYO YA MAGOLI, TIMU YAKE YA BARCELONA HAIKUNYAKUWA KOMBE LA LIGI KUU YA UHISPANIA AY KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI ULAYA MWAKA ULIOPITA.

ABBY WAMBACH, ALISHINDA TUZO KWA UPANDE WA KINA DADA NAYE VICENTE DEL BOSQUE, AKITUZWA KUWA KOCHA BORA.

TIMU BORA YA MWAKA ILIJUMUISHA WACHEZAJI WANAOSHIRIKI KATIKA LIGI YA UHISPANIA PEKEE.

MESSI ALITANGAZWA MSHINDI WA TUZO HIYO YA THE BALLON D'OR, TUZO AMBAYO HUKABIDHIWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA KATIKA SHEREHE ILIYOFANYIKA MJINI ZURICH

MESSI ALIKUWA MIONGONI MWA WACHEZAJI WATATU WALIOTEULIWA NA JOPO LA WANDISHI WA HABARI NA MAKOCHA WA TIMU ZA TAIFA, MANAODHA WA TIMU HIYO WAKIWA NI PAMOJA NA INIESTA NA RONALDO.

MESI SASA NI MCHEZAJI WA KWANZA KUWAHI KUSHINDA TUZO HIYO YA BALLONS D'OR, KWA MIAKA MINNE MFULULIZO, REKODI ANAYOSHIKILIA NA ALIYEKUWA MCHEZAJI WA UFARANSA NA RAIS WA UEFA KWA SASA MICHEL PLATINI.
 

No comments:

Post a Comment