Monday, January 14, 2013

MCHAKATO WA KUMPATA SKAUTI MKUU.



BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/1/13/2013/19:21:17

KAMISHNA WA SKAUTI KATIKA MKOA WA PWANI, BW. HAMIS MASASA AMEMPONGEZA MKUU WA MKOA WA MKOA WA PWANI KWA KUWEZA KUSHINDA NAFASI YA KWANZA KATIKA MCHAKATO WA KUMPATA SKAUTI MKUU WA TANZANIA.

AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI MJINI KIBAHA, KAMISHINA WA SKAUTI MKOA WA PWANI, BW. MASASA AMESEMA KITENDO CHA BIBI. MWANTUM MAHIZA KUONGOZA KATIKA KINYANG'ANYIRO HICHO KWA KUWASHINDA WAGOMBEA WENGINE WAWILI AMBAO WAMEPATA KURA 22 KILA MMOJA AMBAO NI BW.ABDULKARIM SHAH MBUNGE WA MAFIA NA BW. KAJUNGUMJULI KUTOKA MKOA WA MWANZA, AMBAPO BIBI.MAHIZA AMEIBUKA NA KURA 47.

BW. MASASA AMESEMA BAADA YA HATUA HIYO MAJINA MATATU YATAWASILISHWA KWA RAIS WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA, AMBAYE NI WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI BW. SHUKURU KAWAMBWA KAMA UTARATIBU UNAVYOELEKEZA AMBAYE NAYE ATAYAWAKILISHA KWA MLEZI WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DOKTA JAKAYA KIKWETE AMBAYE YEYE ATAKUWA NA JUKUMU LA KUCHAGUA JINA MOJA KATI YA MATATU YALIYOCHAGULIWA ILI KUMPATA SKAUTI MKUU NA BADAYE KUAPISHWA KWA MUJIBU WA TARATIBU.

BW. MASASA AMEELEZEA UWEZO WA BIBI. MWANTUM MAHIZA WA KUPANGA MIPANGO MBALIMBALI YA KUMUENDELEZA KIJANA NA MFANO NI UANZISHAJI WA KAMBI YA MAARIFA ILIYOKUFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MSOGA WILAYANI BAGAMOYO AMBAPO VIJANA WALIKUSANYWA KUTOKA WILAYA ZA MKOA WA PWANI NA KUPATIWA MAFUNZO YA UJENZI WA NYUMBA KWA GHARAMA NAFUU NA KUWEZESHA VIJANA HAO KUPATIWA MASHINE ZA KUFYATUA TOFALI NA MIFUKO 100 YA UDONGO ULAYA.

KWA HATUA HIYO YEYE KAMA KAMISHNA WA SKAUTI MKOA WA PWANI KWA NIABA YA SKAUTI WA MKOA HUO AMECHUKUA FURSA HIYO KUMPONGEZA BIBI. MAHIZA KWA KUWEZA KUONGOZA KATIKA MCHAKATO HUO NA HASA IKIZINGATIWA TOKA AMEFIKA MKOA WA PWANI, AGENDA YAKE KUBWA IMEKUWA NI MAENDELEO YA VIJANA NA KUNA UHAKIKA MKUBWA AKIBAHATIKA KUPATA NAFASI HIYO ATAWEZA KUSAIDIA VIJANA WA NCHI NZIMA BADALA YA WA MKOA WA PWANI PEKEE YAKE.

No comments:

Post a Comment