Tuesday, December 4, 2012

NILISIKIA IMETOKEA HUKOOOO.............

MKE:"Vipi mume wangu mbona leo umerudi mapema nyumbani na una majonzi?"

MUME:"Wenzangu wote wamefariki kulitokea moto ghafla kazini."

MKE:"Mungu wangu...we umeponeaje?"

MUME:"Tumbo lilikuwa linasumbua nakuharisha,nikaenda choo cha ofisi jirani kile cha ofisi yetu ni kibovu,hivyo ndivyo nilivyoponea kifo."

MKE:"Nazionea huruma familia za wenzio sasa wataishije?"

MUME:"Watu wa bima(insurance) wamesema watapatia kila familia Millioni Ishirini."

MKE:"Aagrh! Unaona mambo yako ya kuharisha haya! Umekosesha familia yako Millioni Ishirini!!"

No comments:

Post a Comment