Saturday, December 15, 2012

M4C YATUA KIBAHA


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO KIMEZINDUA RASMI KAMPENI YAKE YA VUGUVGU LA MABADILIKO MJINI KIBAHA KWA KUWATAKA WANANCHI KUCHUKUA HATUA ILI KULETA MABADILIKO AMBAYO YATASAIDIA KUCHOCHEA MAENDELEO YA NCHI YETU.

AKIONGEA KATIKA MKUTANO WA HADHARA KATIKA VIWANJA VYA MPIRA MAILI MOJA, MBUNGE WA UBUNGO, BW. JOHN MNYIKA AMESEMA WAKATI NI HUU KWA WALE WANAOTESEKA KATIKA NCHI HII KUNGA MKONO KAMPENI YA VUGUVUGU LA MABADILIKO ILI KUYAONA MABADILIKO AMBAYO MNATAKA KUYAONA.

BW. MNYIKA AMEBAINISHA KUWA ILI KUWA WAKALA WA MAGEUZI INABIDI KILA MTU AWAJIBIKE KATIKA ENEO LAKE KAMA NI MWALIMU AWE WAKALA WA MABADILIKO KATRIKA ENEO LAKE, NA KAMA NI ASKARI BASI AWE WAKALA WA MABADILIKO KATIKA ENEO LAKE HALIKADHALIKA WAMACHINGA NA JAMII NZIMA KWA UJUMLA.

MBUNGE HUYO WA UBUNGO AMEONGEZA KUWA WANANCHI WAMEKUWA WAKIONA MISUKOSUKO MBALIMBALI IKIWAKABILI VIONGOZI WA CHADEMA, KAMA MAUAJI YA MOROGORO, MAUAJI YA MWANDISHI DAUD MWANGOSI, YALIYOMKUTA DR. ULIMBOKA NA KUFUNGIWA GAZETI LA MWANANCHI HIZO NI DALILI TOSHA YA KWAMBA UTAWALA UMESHINDWA KUONGOZA NCHI KWA MAARIFA.

KABLA YA KUHUTUBIA MKUTANOI HUO VIONGOZI WA CHADEMA WAKIONGOZWA NA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO MJINI KIBAHA, BW. SENKONDO BUMIJA NA WABUNGE SUSAN KIWANGA, CECILIA PEROSA, EZEKIEL WENJE, MCHUNGAJI MSIGWA WALINADI VYEMA MIKAKATI YAO YA KUCHUKUA DOLA ITAKAPOFIKA MWAKA 2015.

AIDHA MSAFARA HUO ULIZINDUA UJENZI WA ZAHANATI ENEO LA MSANGANI NA KUCHANGIA PAPO KWA PAPO MIFUKO 20 YA UDONGO ULAYA ILI KUSONGESHA MBELE UJENZI WA ZAHANATI HIYO INAYOJENGWA KWA NGUVU ZA WANANCHI WA MTAA MSANGANI, MTAA AMBAO UNA MWENYEKITI WA SERIKALI KUTOKA CHADEMA, BW. ALLY GONZA, AMBAPO WAO KAMA WAO WAMEWEZA KUFYATUA MATOFALI 500 KAMA HATUA YA KUMUUNGA MKONO MWENYEKITI WAO.

No comments:

Post a Comment