Saturday, December 15, 2012

KULE: ARSENAL WANA MWAKA MMOJA NA NUSU KUSUBIRI WENGER AMALIZE MKATABA WAKE


MAISHA YA KOCHA, ARSENE WENGER, KWENYE KIKOSI CHA ARSENAL YANAZIDI KWENDA KOMBO NA HUENDA SAFARI HII MAJI YAKAZIDI UNGA.

HIYO NI KWA KUWA BILIONEA, ALISHER USMANOV, AMBAYE NI MWANAHISA WA KLABU HIYO HATAKI KUMWONA KOCHA HUYO NA BADALA YAKE AMEPENDEKEZA SHUJAA WA ARSENAL, THIERRY HENRY, ATUE KATIKA KLABU AKIWA KAMA KOCHA.

ARSENAL KWA SASA IMEKUWA IKIFANYA VIBAYA KATIKA LIGI NA JAMBO HILO LIMEFANYA MASHABIKI NA HATA VIONGOZI WA KLABU WACHUKIE MBINU ZA WENGER ZA UFUNDISHAJI.

"THIERRY ANATAKIWA AJUMUISHWE KWENYE KLABU HII, LAKINI SI KAMA MCHEZAJI, ANATAKIWA KUFIKA HAPA AKIWA KOCHA," ALISEMA BILIONEA KUTOKA RUSSIA, USMANOV.

"ANATAKIWA KUTOA UJUZI WAKE KWA WATU WENGINE. BADO ANA KAZI KUBWA YA KUFANYA KWENYE KIKOSI HIKI."

USMANOV AMBAYE ANA ASILIMIA 29 YA HISA KWENYE KLABU HIYO, AMESEMA HENRY ATAWASAIDIA KUONDOKANA NA MATATIZO WANAYOKABILIANA NAYO SASA.

JAMBO JINGINE LINALOONGEZA VUGUVUGU KWENYE KLABU HIYO NI MATAMSHI YA MAKAMU WA RAIS, NINA BRACEWELL-SMITH AMBAYE ALIUZA HISA 15 KWA STAN KROENKE WA MAREKANI.
BRACEWELL-SMITH ALIULIZA IWAPO KROENKE ANAYENG'ANG'ANIA WENGER AWEPO KAMA ANAIPENDA KLABU.

BRACEWELL-SMITH, ALISEMA: "NI KWELI WENGER AMETENGENEZA FEDHA KWENYE KLABU, LAKINI HICHO SI KIGEZO PEKEE CHA KOCHA HUYO KUENDELEA KUWEPO.

"SOKA LINAJUMUISHA VITU VINGI IKIWA NI PAMOJA NA HISIA ZA WATU. STAN KROENKE WALA HAVUTIWI NA SOKA NDIO MAANA ANAONA MAMBO YOTE NI SAWA TU."

MKONGWE WA ARSENAL, HENRY MWENYE UMRI WA MIAKA 35 NA WAKALA WAKE DARREN DEIN AMBAYE NI MTOTO WA MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA ARSENAL, DAVID DEIN, WAMEALIKWA MOSCOW KUFANYA MAZUNGUMZO NA USMANOV.

JAMBO HILO LIMEKUJA SAA 24 BAADA YA TAARIFA KUWA UHUSIANO KATI YA WENGER NA MSAIDIZI WAKE STEVE BOULD SI MZURI.
BOULD ANA HASIRA NA WENGER KWA KUWA HAPEWI NAFASI KUBWA YA KUFANYA KAZI YA UKOCHA.

USMANOV AMBAYE AMEKUWA AKITAFUTA MADARAKA MAKUBWA KWENYE BODI ALISEMA: "SINA NGUVU NYINGI KWENYE BODI LAKINI NINAWEZA KUWAPA KAZI WATU NINAOWATAKA.

NIMEFANYA MAWASILIANO NA THIERRY LAKINI ANATAKIWA KUJUMUISHWA KWENYE KLABU KAMA KOCHA NA SI MCHEZAJI.

UKIANGALIA PATRICK VIEIRA AMBAYE SASA YUPO MANCHESTER CITY ANAFANYA KAZI VIZURI, HILO NI ZAO LA ARSENAL LAKINI ANAISAIDIA KLABU NYINGINE. HATUTAKI KUONA THIERRY AKIPOTEA KAMA VIEIRA."
AWALI WENGER ALIMTAFUTA HENRY KUTOKA NEW YORK RED BULLS ILI AMSAJILI KWA MKOPO.


WAKATI VUGUVUGU HILO LIKIENDELEA, JINA LA WENGER LIMO KATIKA ORODHA YA MAKOCHA WANAOSAKWA NA REAL MADRID. HIYO NI IWAPO JOSE MOURINHO ATAONDOKA.

RAIS WA REAL MADRID, FLORENTINO PEREZ AMEKUWA AKITAMANI KUFANYA KAZI NA KOCHA HUYO WA UFARANSA.

HATA HIVYO WENGER AMESEMA HATAKI KUVUNJA MKATABA ARSENAL KWA KUWA BADO ANA MIEZI 18 YA KUINOA.

No comments:

Post a Comment