Saturday, December 15, 2012

BIBI RICE AOMBA ASITEULIWE NA OBAMA


BALOZI WA MAREKANI KATIKA UMOJA WA MATAIFA SUSAN RICE AMEMWOMBA RAIS BARRACK OBAMA ASIMTEUE KAMA WAZIRI WA MAMBO YA NJE, BAADA YA KUKASHIFIWA VIKALI NA WABUNGE WA REPUBLICAN KUHUSU MATAMSHI YAKE KUHUSU SHAMBULIZI LILILOTOKEA KATIKA UBALOZI WA MAREKANI MJINI BENGAZI NCHINI LIBYA.
RICE AMBAYE NI MSHIRIKA WA KARIBU WA RAIS BARRACK OBAMA ALIKUWA AMEPEWA NAFASI KUBWA YA KUMRITHI HILLARY CLINTON AMBAYE ANASTAAFU MAPEMA MWAKA UJAO BAADA YA KUHUDUMU KATIKA WADHIFA HUO KWA MIAKA MINNE ILIYOPITA.

Balozi wa Marekani katika  Umoja wa Mataifa  Susan Rice

BALOZI HUYO AMEMWANDIKIA BARUA RAIS OBAMA AKIMWAMBIA AKIMTEUA HUENDA KUTHIBITISHWA KWAKE KATIKA BUNGE LA MAREKANI KUKACHUKUA MUDA MREFU NA ATAPATA VIKWAZO KUTOKA KWA WABUNGE WA REPUBLICAN JAMBO AMBALO ANAONA HUENDA LITALIGAWA TAIFA HILO.
WACHANBUZI WA SIASA ZA MAREKANI WANAONA KUWA RAIS OBAMA AMESHINDWA KUMPIGANIA NA KUMTETEA RICE DHIDI YA SENETA JOHN MCCAIN AMBAYE AMEKUWA KATIKA MSTARI WA MBELE KUMKOSOA RICE.
RICE ALINUKULIWA AKISEMA KUWA YALIYOTOKEA NCHINI LIBYA YALIKUWA NI MACHAFUKO YA PAMOJA NA SHAMBUZLI DHIDI YA BALOZI WA MAREKANI HUENDA HAYAKUPANGWA KWA MUJIBU WA TAARIFA YA KIUSALAMA MATAMSHI AMBAYO WABUNGE WA REPUBLICAN WANAKOSOA VIKALI.
RAIS BARRACK OBAMA ANAKUTANA NA RICE IJUMAA HII KATIKA IKULU YA WHITE HOUSE KUJADILI KWA KINA OMBI LAKE LA KUTAKA KUTOTEULIWA KWAKE KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE.
AIDHA, RAIS BARRACK OBAMA ANATARAJIWA PIA KUMTAGAZA WAZIRI MPYA WA ULINZI ATAKAYECHUKUA NAFASI YA LEON PANETTA PAMOJA NA KIONGOZI WA IDARA YA UJASUSI NCHINI HUMO CIA.

No comments:

Post a Comment