Sunday, November 4, 2012

HABARI ZA UAMSHO ZANZIBAR


Meneja wa Baraza la Habari kanda ya Zanzibar(MCT)Suleiman Seif Omar akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu tamko la Tume ya utangazaji Zanzibar kupiga marufuku kuripoti taarifa za UAMSHO zenye kuashiria uvunjifu amani kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John P.Mireny
………………………….
Na Maelezo Zanzibar
 Vyombo vya habari nchini vimeshauriwa kujiepusha kuandika habari za uchochezi zinazoweza kuhamasisha chuki ndani ya jamaii na hatimaye kuvuruga amani na utangamano wa nchi.
 Ushauri huo umetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanaznia (MCT) John Mireny alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Baraza hilo Mlandege Zanzibar kuhusiana na Tamko lililotolewa na Tume ya Utangazaji Zanzibar la kupiga marufuku matangazo yote yanayohusiana na vurugu zinazohusishwa na wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO Zanzibar.
 Amesema pamoja na ukweli kwamba Baraza la Habari linatambua na kutetea kwa nguvu zote uwepo wa uhuru wa Vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza, Baraza linasisitiza kwamba vyombo hivyo vinawajibu mkubwa wa kulinda amani na jamii kwa ujumla.
 Amesema Tume haikukosea kupiga marufuku taarifa za Jumuiya ya UAMSHO zinazoashiria fujo na uvunjifu wa amani na kwamba hizo ni taarifa ambazo hazikubaliki kutolewa katika vyombo vya habari.
 Hata hivyo ameongeza kuwa taarifa zinazohusu UAMSHO ambazo hazihusiani na fujo na uvunjifu wa Amani zinaweza kutolewa na vyombo vya habari nchini ili kuipasha jamii habari za Jumuiya hiyo.
 Ametoa mfano wa habari za Jumuiya ya UAMSHO ambazo zinaweza kuripotiwa kuwa ni pamoja na mwendelezo wa Kesi inayohusu Viongozi waandamizi wa Jumuiya hiyo Uchimbaji wa Visima habari za kimaendeleo uchumi na kadhalika .

No comments:

Post a Comment