WAKUU WA GUINEA WANASEMA KUWA WATU KAMA 30 WAMEKUFA KWENYE AJALI YA
MASHUA KATIKA BAHARI YA ATLANTIC.
INAARIFIWA KUWA MASHUA
HIYO ILIKWENDA MRAMA KWA SABABU YA DHORUBA WAKATI IKISAFIRI KUTOKA MJI MKUU,
CONAKRY, KUELEKEA KISIWA CHA KASSA, SAFARI YA KILOMITA 10.
SHUGHULI ZA UOKOZI
ZIMESIMAMISHWA.
AJALI KAMA HIZO
ZINATOKEA MARA KWA MARA NCHINI GUINEA NA KWENGINEKO AFRIKA, AMBAKO MASHUA
HUPAKIA ABIRIA WENGI NA HAZITAZAMWI SAWA SAWA.

No comments:
Post a Comment