Monday, August 20, 2012

SENSA YAMTOKEA PUANI MKUU WA WILAYA YA KILWA;


 

MKUU WA WILAYA YA KILWA MH ABDALLAH ULEGA AMENUSURIKA KIPIGO KIKALI TOKA KWA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM BAADA YA KUWAHAMASISHA KUSHIRIKI KATIKA ZOEZI LA SENSA. MKUU HUYO WA WILAYA YAMEMKUTA HAYO ALIPOPEWA KIPAZA SAUTI AWASALIMIE WAISLAM BAADA YA KUMALIZIKA KWA IBADA YA SWALA LA IDI-FITRI KATIKA MSIKITI WA AZHAAR ULIOPO KILWA KIVINJE. MHESHMIWA BADALA YA KUTOA SALAM ZA IDI,AKAANZA KUWAHAMASISHA WAISLAM KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA. HATA HIVYO WAUMINI WALIPOTAKA KUMUULIZA MASWALI MHESHMIWA HAKUWA TAYARI NDIPO WAUMINI WALIPOAMUA KUMVAMIA KWA LENGO LA KUMPA KIPIGO. HATA HIVYO POLISI NA USALAMA WA TAIFA ILIBIDI WAINGILIE KATI KUMNUSURU NA KIPIGO,

AKIONGEA BAADAE KATIKA BARAZA LA IDI,BW ULEGA ALISEMA HIVI SASA SITAZUNGUMZIA SWALA LA SENSA KWAKUWA SITAKI KUWAKWAZA TENA WAISLAM. MHESHMIWA ALIWATAKA WAISLAM KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA UKUSANYAJI WA MAONI KWA AJILI YA KATIBA MPYA PINDI TUME ITAKAPOWATEMBELEA.

WAISLAM TANZANIA WAKIWAKILISHWA NA TAASISI ZAO ZOTE IKIWEMO BAKWATA CHINI YA MUFTI SIMBA WALIKUBALIANA KUGOMEA ZOEZI LA SENSA HADI KIPENGELE CHA DINI KITAKAPOINGIZWA KATIKA DODOSO LA MASWALI YANAYOHUSIANA NA ZOEZI HILO. MADAI HAYO WAISLAM YAMETOKANA NA BAADHI YA TAASISI ZA SERIKALI NA KIDINI(KANISA KATOLIKI) KUTOA TAKWIMU ZA IDADI YA WATANZANIA KILINGANA NA DINI ZAO.

HATA HIVYO SIKU CHACHE BAKWATA WALIJITOA KATIKA KUNDI HILO LA WAISLAM NA SASA INASHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUWAHAMASISHA WAISLAM KUSHIRIKI KATIKA ZOEZI LA SENSA.

No comments:

Post a Comment