Sunday, July 8, 2012

WAKIMBIZI WA ZANZIBAR WAREJEA


MOHAMMED,MAELEZO ZANZIBAR
WATANZANIA 35 KATI YA 38  WALIOKUWA WANAISHI UKIMBIZINI JIJINI MOGADISHU NCHINI SOMALIA WAMEWASILI SALAMA KISIWANI PEMBA KUANZA MAISHA MAPYA BAADA YA KUISHI KAMA WAKIMBIZI KWA MIAKA 12.
AFISA MSAIDIZI ANAYEHUSIKA NA USHIRIKISHWAJI HABARI NA UMMA WA SHIRIKA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI LA UMOJA WA MATAIFA OFISI YA TANZANIA, AUSTIN MAKANI ALISEMA WATANZANIA HAO WAMEWASILI BANDARI YA MKOANI MKOA WA KUSINI PEMBA JANA SAA 5.00 ASUBUHI WAKITOKEA UNGUJA NA BOTI IENDAYO KASI YA SEA BUSS III.
MJINI UNGUJA,WALIFIKIA HOTELI YA BWAWANI WALIKOLALA KWA USIKU MOJA KABLA WALIPOGAWANYWA WAKAAAZI WA PEMBA 35 WALIANZA SAFARI ILIYOWACHUKUA HADI CHAKE CHAKE NA WALE WA UNGUJA WALIKABIDHIWA KWA MAMLAKA ZA SERIKALI.
WATANZANIA HAO WAKIWA NA FAMILIA ZAO WENGINE WAKIWA WAMESHAOA RAIA WA SOMALIA NI 35 AMBAO NI WAKAAZI WA PEMBA,WATANO WANAISHI UNGUJA NA KUFANYA IDADI YA WALIOREJEA KWA HIARI YAO KUTOKA SOMALIA NI 38.
 JUZI, NDEGE MBILI ZA UMOJA WA MATAIFA ZINAZOHUSIKA NA HUDUMA ZA KIBINADAMU  ZILIWABEBA RAIA HAO WA TANZANIA WAKITOKEA SOMALIA WALIWASILI  UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA ABEID AMANI KARUME SAA 8:15 MCHANA WAKIWA NA SIHA NJEMA NA WENYE FURAHA WALIPOKELEWA NA MAOFISA WA UNHCR OFISI YA TANZANIA.
MKUU WA MKOA WA KUSINI PEMBA, MEJA MSTAAFU JUMA KASSIM TINDWA ALIWAPOKEA WANANCHI HAO KATIKA BANDARI YA MKOANI AKIWAELEZA KUWA WAMEFANYA UAMUZI WA BUSARA KUREJEA NYUMBANI KUUNGANA NA FAMILIA ZAO NA WATANZANIA WENGINE KATIKA UJENZI WA TAIFA.
KATIKA BANDARI YA MKOANI LICHA YA ENEO LAKE KUWA DOGO, WANANCHI WENGI WALIJITOKEZA KUWALAKI RAIA WENZAO AMBAO HAWAKUWAONA KWA MUDA WA MIAKA 11 SASA WALIOKUWA WAMEKIMBIA VURUGU ZA KISIASA ZILIZOTOKEA JANUARI 26 NA 27 ZILIZOSABABISHA WATU KADHAA KUPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUKIMBIA MAKAZI YAO.
MAKANI ALISEMA MWISHO WA SAFARI NA HUDUMA ZA UNHCR NI WILAYA YA CHAKE CHAKE MKOA WA KUSINI PEMBA AMBAPO KUANZIA HAPO MKATABA WAO WA KUWAHUDUMIA UTAKUWA UMEMALIZIKA NA WATAHESABIKA KUWA NI RAIA WENGINE WA KAWAIDA WAKIUNGANA NA FAMILIA ZAO.

No comments:

Post a Comment