Thursday, July 5, 2012

"SAYANSI MBADALA" YAMUUMBUA DADA HUYU


 

MWANAMKE HUYU AMBAYE HAKUFAHAMIKA JINA LAKE AMEKUTWA KATIKA MAZINGRA HAYA JANA ALFAJIRI MAENEO YA ILOMBA JIJINI MBEYA AKIWA KAMA ALIVYOZALIWA, INADAIWA KUWA MWANAMKE HUYU NI MMOJA WA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA TEOFILO KISANJI(TEKU).

WANANCHI WALIKUSANYIKA KATIKA ENEO ALIPOKUTWA MWANAMAMA HUYU AMBAPO INADAIWA KUWA ALIKUWA AKIWAQNGA NYAKATI ZA USIKU LAKINI AKAKUTANA NA WABABE WA ULOZI MITAA HIYO NDIPO ALIPOSHINDWA KUENDELEA NA ULOZI WAKE NA KUJIKUTA AKIKOSA NGUVU NA KUSHINDWA KUENDELEA NA SAFARI YAKE YA ULOZI HADI ALIPOKUTWA ASUBUHI KWEUPEE!!!

INAELEZWA KUWA ENEO HILO NI MAARUFU KWA KUKAMATA WATU WANAOINGIA ANGA HIZO KWA AJILI YA KUFANYA UGAGULA AMBAPO MIEZI MICHACHE ILIYOPITA MTOTO MDOGO WA KIKE NAYE ALIBAMBWA AKITAKA KUFANYA ULOZI NA KUKUTWA NA UMATI WA WATU KABLA YA KUFANYA ULOZI WAKE.

MWANAMKE HUYU ALIOKOLEWA NA ASKARI POLISI AMBAO WALIMCHUKUA MOJA KWA MOJA HADI KITUONI KWA AJILI YA KUHIFADHIWA ILI ASIPATE MADHARA ZAIDI.JITIHADA ZA KUKUTANA NA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA TEKU ZINAENDELEA ILI KUJUA KAMA MWANAMKE HUYU ALIKUWA NI MWANAFUNZI WA CHUO HICHO KAMA INAVYOELEZWA NA WATU AMA LA.

No comments:

Post a Comment